Logo Design by FlamingText.com
Logo Design by FlamingText.com

storynzuri sehemu ya hamsini na tatu shemeji ingiza pole pole



.
.
Sehemu ya Hamsini na Tatu
Mtunzi INSTAGRAM @hanscharlz @storynzuri
.
ilipoishia "Na nilikuwa makini sana pindi niingiapo na kutoka kwani sikupenda sana endapo shem Erinest akiniona nami nilikuwa makini mnooo na kuhakikisha hanioni kwani nilihisi anataka kupajua mahari napo ishi tu si vingine.
.
Siku hoyo ilikuwa nzuri sana kwangu kwani daktali aliniita ofisini na kuanza kusemezana nami na huku akionekana kutaka kunipa habari njema ambazo mimi sikuwa nazijua.
"aaahaaah Isabela leo nina habari nzuri mno kwako?"
"Habari ipi tena dokta mbona wanitia wasi wasi mwingiiiiiii nambiyeee nami nijue?"
Ndipo nilipo kwisha kusema hayo nae alionekana mwachoni mwangu akitoa tabasamu kama la kipindi cha nyuma nami nilipo rudisha fikira zangu nyuma na kujua tu hizo taharifa zitakuwa zimelenga sana kwa Erick mgonjwa wangu. Lakini sikutaka kuamini sana mpaka hapo atakapo sema mwenyewe ndipo nilipokuwa nikifikiria hayo nae aliendelea kusema.
"Ni kuhusu mgonjwa wako Erick leo kwa mujibu wa vipimo nilivyokuwa nimemuchukua ana kila sababu ya kupata ruhusa ya kwenda kupata au kumalizia matibabu nyumbani kwa afya yake iko imara kwa sasa lakini unashauliwa kuzingatia yafuatayo?
Chakula bora
Matunda na mboga mboga kwa wingiii ili kurudisha afya yake kuwa kama zamani na pia Mazoezi muhumu kwake anatakiwa kuwa anafanya japo yasio ya kutumia nguvu sana bali ya kawaida tu kwani mwili wake utaimalika pia kwa hivyo nilivyo kuwambia vifanyie kazi na majibu utayapata hakika UTANIPENDA Isabela"
"sawa daktali wala usijali kwa hilo kwani nitakuwa makini sana kwa ujumbe huuu ulioniambia hakika nitazingatia na kuufanyia kazi ipasavyooo lakini daktali samahani eti Erick anatoka saa ngapi au ni mda huuu! nijuze nami nijue tafadhari daktali!!!!!!1

"Haaaaaah Isabela ruhusa hiiii ni kwanzia sasa navyo ongea iko tayari inafanya kazi na kwenye faili nimesha andika na kinacho takiwa wewe kama unataka kwenda sasa ni kufika alipo lazwa Erick na umchukue mwende kwenye mapumziko ya nyumbani lakini dawa tu nasisitiza"
"Sawa daktali"
Nilitoka ofini mwa daktali huyo nikiwa na furaha nyingi ya kuwa Erick kwa sasa atakuwa kapona basi huku nikiwa na sipindi na furaha iliokuwa imejaa kifuani kwangu nilifika mpaka alipokuwa kalazwa Erick na kutazama kwenye kitanda hakuwepo lakini kumbe alikuwa yuko pemebni kidogo mwa kitanda kakaaa akiwa mchangamfuu. Nilifika mpaka alipokuwa amekaa na kuanza kusemezana nae huku nikizitazama nyuso zake.
"mambo Erick"
"poa"
"Vipi hali yako maana daktali huko katoa ruhusa yako ya kwenda kumalizia matibabu nyumbani"
"mimi naendelea vizuri kama daktali alivyo kuambia kwani nami nilikuwa nasubilia tamko tu la lini na siku gani kuruhusiwa kurudi nyumbani lakini kama kakwisha kukufahamisha sina budi ngoja nichukue kilicho changu hapo na sio vingi ili tuongozane wote"
"sawa Erick wala usijali tutaongozana tu"

Aliniacha pale na kwenda kwenye kitanda alichokuwa akilala akabeba nguo aliokuwa akitumia kipindi chote alicho kuwepo hapo hospitali na kurudi nilipokuwa na kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwake licha ya kujiwekea asilimia mia za kuwa tunaenda kwake japo sikuwa na huakika wa jambo flani ambali dakika chache ningejua jibu lake?
Tulitoka mpaka maeneo ya nje ya hospitali na ndipo nilipo mwacha mahari apumzike nami ili niweze kwenda kuita bajaji ili itupeleke tutakako. Nilifanya hivyo nami nilipata bajaji na kurudi tena alipo Erick ili kumchukua na kwenda nilifika alipo kuwa Erick na kupanda na kuanza safari lakini katikati ya safari Erick alimuelekeza dereva wa bajaji mahari anapo paswa kutupeleka. Haikuchukua mda sana na tulipokuwa tunakwenda tulifika na niliposhuka tu kwenye aridhi hiyooo Erick alionekana kukaa/kuishi mahari pa wenye pesa zao chafuuu yaani matajiri huku nikibaki nikijisemea moyoni kuona nyumbani nzuri zikizunguma maeneo hayo na kuanza kujiuliza ipi ya Erick?

Nilimpatia dereva pesa yake ya usafiri nae aliondoka na ndipo sauti kutoka kwa Erick ilisikika
"Karibu sana Isabela huku ndiko ninako ishiii mimi na hapo mbele ndipo kwanguuu, Nilishitushwa sana na nyumba alionionesha kwani ilikuwa ikionekana kuwa nyumba nzuri mtaa mzima lakini ilikuwa kwa macho yangu tu. Basi nami nilimjibu Erick kwa kunikaribisha vizuri.
"Asante sana Erick nimesha karibia"
Tuliongozana mpaka kwenye geti nae alogonga na kutoka kijakazi kufungua mlango
"Bosi ulikuwa wapi siku zote watu tumeishi bila amani humu huku simu yako pia haipatikani kulikoni boss?????"
Erick "Nilipata matatizo lakini ngoja nipumzike kidogo nitakufahamisha yote lakini mpaka nitakapo amka sawa"
kijakazi "sawa boss karibu sana na pole na matatizo japo sijayafahamu"
Nilibaki kuwa bubu huku nikiwaacha wakiendelea kuzungumza huku mimi nikimfata tu kwa nyuma mwenyeji wangu Erick. huku nikimfata hivyo hivyo nilijishitukia niko sebureni nae alipokwisha nikaribisha pia sebureni nae alichomoka na kwenda kwenye vyumba vilivyo kuwa vime karibiana na sebulehuku nami nikimgojaaa atokealipokuwa kaenda ili tukae tuonge vizuri lakini niliingiwa na hofu pale alipokuja na mtu wakiwa wameongozana nao walifika na kukaa kwenye makochi na ndipo Erick akachukua jukumu la kumtambulisha mtu huyooo?

JE NI NANI HUYOOO BASI USKOSE SEHEMU YA 54 HAPA HAPA KUJUA NI NANI?

STORY WRITER HANS

FOLLOW INSTAGRAM @storynzuri 

.....................S T A R...B O Y ....................................



















Share on Google Plus

About storynzuri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

4 comments: