.
.
Mtunzi INSTAGRAM @hanscharlz @storynzuri
.
.
Ni story inayo muhusu binti mmoja akizama kwenye penzi zito
la kijana muuza nguo waswahili wanapenda kumuita (machinga) kijana Hans
Ni kipindi cha nyuma sana na ni takiribani mwaka mmoja umepita
sasa tangu familia ya mama na baba happy kupata mtoto happy na kumsomesha mpaka
hapo alipo fika masomo yake ya ngazi shule ya msingi na kumaliza na alipo
maliza alirudi nyumbani huku akisubiria matokeo ya kufuzu na kuendelea na
masomo.
Ilikuwa siku moja asubui mama happy aliamka na kumwamsha
happy ili afanye usafi na kumsimamia dada wa kazi kuhakikisha mazingira
yanakuwa mazuri
Mama “happy happy happy!!!!!!!! hamka kumekucha sawa
mwanangu”
Happy “mmmmmmh mama mbona mapema sana hivi”
Mama “mda huuuu ni saaa kumi na mbili 12:30 hamka mwanangu
ukamwangalie dada huko nje”
Happy “sawaaaaaa!!!! Mama ngoja nivae nguo”
Mama “okay fanya hivyo hakikisha kila kitu kinaenda sawa”
Happy “sawa mama”
Happy aliamka na kuelekea alipokuwa mama kamwambia na kutoka
mpaka nje na alikuwa amesimama nje kabisa ya nyumba yao asubui na mapema huku akiendelea
kumsimamia kijakazi wao wa ndani kufanya usafi usafi unaozunguka nyumba yao pia
na ndani walikuwa wamekwisha maliza...”
Happy; “huo mchanga mbona unaukwepa, kulikoni tena! Heeee
ila naomba ufagilie pembeni.”
Dada; “Sawa.”
Happy “Halafu hicho si ni mabaki ya chakula kwa nini unaweka
hapo badala ya kwenda kutupa jalalani”
Dada “Haya mabaki ya chakula
kuna mtu anakujaga kuchukua.”
Happy “Kuna mtu anakujaga kuchukua? Na husema anapeleka wapi?”
Dada “Anakwenda kuuza kwa wauza mabaki hayo lakini
sijamuuliza vizuri lakini ndio hivyo?”
Happy “Mh! Kwani siku hizi na mabaki ya chakula yana
biashara yake?
Dada “Nasikia hivyo,” alijibu msichana wa kazi.
“Itakuwa ni kwa ajili
ya kazi nyingine lakini si kuuza,? alisema happy.
Ni kweli, happy asingeweza kujua kama mabaki ya chakula ni biashara kubwa sana mjini kwa sasa kwa
sababu binti huyo huwa hatoki sana kutembeatembea nje. Kwani huwa akitoka na
gari la familia kwenda saloon na viwanja vikubwa. Na akirudi tu nyumbani
hushinda ndani tu.
.
.
Tangu amemaliza masomo yake ya elimu ya juuu huku akisubiri
mambo mengine yatakayo tokea, yeye amekuwa akitumia muda mrefu sana nyumbani kutazama
muvi kiasi kwamba hata wazazi wake wamekuwa wakimsema na kumwonya ya kwamba
anaweza kupofuka macho na kuleta shidaaa siku za mbeleni lakini happy alikuwa
hata kuwaelewa wazazi wake yeye aliona sawa tu.
Baada ya msichana wa kazi kumaliza usafi wan je na
kuhakikisha kaweka vizuri mazingira na waliingia ndani. Alitangulia msichana
huyo wa kazi na , Linda akafuata nyuma huku akitizama kuwa kazi aliyo ifanya
siku hiyo binti huyo wa kazi hakuwai fanya kipindi cha nyuma huku akijisemea
asinge fanya hivyo?.
Basi Ile anafunga mlango tu ili kuingia ndani , mara geti likagongwa...
“Kokooo kokoooooo kokooooooo.”
Ilionekana kuwa mgongaji alikuwa akitumia funguo, au kitu
cha chuma chochote kile. Ndipo alipogeuka na
Happy akafungua... geti hilooo na kumtazama na kumuona
kijana
“Samahani anti, namuulizia.”
Happy hakutaka kusubiri hadi litajwe jina la huyo anayeuliza
akafunga geti kwa nguvu na kuegemea kwa ndani akihema kwa nguvu...
“Dada nini” msichana wa kazi aliuliza huku akiwa na hofu
maana alivyooo ufunga geti hilo alishituka sana.
“Kichaa.”
“Kichaa!”
“Kichaa kabisa kabeba limfuko.” Happy alimwambia dada wa
kazi?
“Atakuwa anataka nini?”
“Eti sijui anamuuliza nani, maana nilivyooo mwona tu mi
sikutaka hata kumsikiliza.?
Mgonga geti alipoona hali ile aliondoka zake huku
akisikitika...huku akiacha lawama nyingi!
“Mademu wengine bwana daaah!, anajiona yeye ni matawi sana,?
alisema moyoni mtu huyo. Aliteremka eneo la bonde na kutokea kwenye jalala
ambapo aliokota vyakula vilivyokuwa vimemwagwaaa.
.
.
Ndipo walipo fika ndani huku happy akiwaza kichaa kichaaaa
na alipo mwona mama yake nae alimkimbilia nan a kwenda kutoa mashitaka
(malalamiko)
“Mama, mwenzio kidogo nifanyiwe kitu mbaya na kichaa,”
alisema happy.
“Na nani?” mama aliuliza huku akiwa na jaziba pindi
alipopokea malalamiko hayo?
“Kichaa.” Happy alijibuu
“mmmmmh mwanangu Ilikuaje? Na kakuzuru mwanangu
“Sisi tulikuwa tunaingia ndani, name nilikuwa nyuma na mtu
wa mwisho lakini ile nafunga geti tu mtu akagonga, kufungua hee! Kabeba mfuko
mchafu mgongoni, akasema anamuulizia nani sijui, mi sikutaka hata kumsikiliza maana
niliogopa sana”
“Isijekuwa ni wale vijana waokota mabaki ya chakula !?
“Mh! Mama! Mwokota vyakula ndiyo atakuwa mchafu vile?” happy
aliulizaaa
“Kwani we hujawahi kuwaona. Wanakuwa wachafu kwa sababu ya
kutembea kwenye majalala kila wakati na kwenye nyumba za watu wachache wanao
jua kuwa wanaweza kupata watakacho?
“Mh! Sasa ndani alitaka nini maana daaah alinifanya
nichanganyikiwe mda huo?”
“Labda alitaka kumuulizia johari mahari alipo weka mfuko
alioweka, si ndiyo anaye mwonyesha anapoweka vyakula hivyo?”
“Aaa! Ndiyo kumbe kuna mfuko hapo njee uliokuwa umesheheni
alichotaka?”
“Eee. Kwani hamkuwa wote na johari?”
“Nilikuwa naye lakini alikuwa amesha ingia ndani na
hakumwona nilimwona mwenyewe tu.”
“Basi atakuwa yeye.” Mama alimaliza kwa kumwambia hivyo.
Mwezi na siku zilipita, siku moja happy alikuwa akitoka na
gari kwenda kupiga miseleeeeee!!!!! kama
alivyooo zoea . Ile anamalizia geti tu, yule kichaa alionekana kwenye uso wa
binti happy. Happy alitetemeka sana aliamini mtu huyo anaweza kuokota mawe na
kulitupia Gari Lake..........! hofu ilitandaaa na kila akizidi kumona.
“lakini huyu si ndiyo yule aliyemsema mama?” alijiuliza
happy...
“lakini Ni mwenyewe na ule mfuko si una vitu” Atakuwa ni
huyu tu.?
Happy alijipa ujasiri kwa kufungua kioo cha gari cha upande
wake na kuchungulia nje... na kuanza kumuuliza kijana huyoooo.
“Za leo ma mdogo?”
“Nzuri tu, mzima?”
“Mi mzima. Vipi yulee demu yupo?”
“Demu gani? Tena huyooooo”
“Kuna demu anaishi ndani humo, mzuri kama maji ya kunde hivi, anapenda kuvaa
magauni marefu na yenye heshimaaa?
Haapy nae alijua ni johari kwa sifa hizo alizo kuwa
akimtunuku demu aliye kuwa akimsemaaa?
“Yupo. Wa nini?” aliuliza happy
“Nataka nimshukuru kwa ule mfuko alikuwa kauweka pale nje
huwa ananiwekea mimi.?
“Ooo! Nitamfikishia salamu zako, we chukua mfuko tena kama
upo nenda.”
“Poapoa anti.”
Nae alipotaka kuondoka tu happy alimuuliza kijana huyooo
“Unaitwa nani?”
“Hans.”
“Hans” Hans nani?”
Hans nae alionekana kuwa mbishi kwa kumjibu happy huku
akisema
“Aaa anti, mbona maswali gani hayo, we jina la mbele la nini
kwanza??
Happy alimwangalia kijana huyo kwa muda mrefu sana. Bado
aliamini hata kama ni suala la kufika kila wakati jalalani lakini ana ukichaa
kwa mbali...? yote hayo alijiuliza na kujijibu mwenyeweee
“Huyu lazima kichwani hakuna network kwani yaonekana kuwa
hayuko vizuri. Mwangalie kwanza, ona! Hajali, hajitambui. Maneno hayo yote
aliyaongea binti happy pindi alipokuwa akimtizama sana Hans?
Na ndipo alipo chukia na kutamka maneno mabaya mno binti
happy “Kwanza mwisho leo kuja kuokota c hapa, nitamwambia johari awe anakwenda
kuzitupa jalalani,” alisema happy huku akikanyaga mafuta na kuondoka maeneo ya
nyumbani huku Nyuma, yule kijana alikwenda kugonga geti nyumbani kwa wakina
happy na ndipo Johari alisikia na alitoka njee.
“Mambo?” alisalimia johari.
“Poa, halafu mbona kuna demu mmoja humu ndani kwenu
ananimaindi sana kulikoni mbona anakuwa na shobo ambazo hazina maana yoyote.”
“Yule ni dada, mtoto wa mwenye nyumba na mimi pia
ananiendesha sana lakini natafuta nitafanya nini lazima nitiiii tu. Si unawajua
wasichana wa kitajiri mambo yaooo?”
“Ah! Ananimaindi sana.
Lakini Katoka hapa mda hiii na nilikuwa nakuulizia wewe
sijui kanijibuje sijui, yaani na mimi nammaindi vilevile kama yeye
anavyonimaindi mimi!?
“Usimjali. Unajua alikuwa chuo, karudi sasa lakini hana
neno.” Johari alimpa moyo kijana hans
“Vipi, mama yupo?” hans aliuliza
“Yupo ndani.”
“Mzigo leo vipi?” hakusahau mzigo nao aliulizia hans
“Mzigo si ule pale nimekuwekea tena leo niliuweka vizuri
wewe nenda kauchukue tu”
“Niuchukue?”
“Si nimekuwekea wewe, kauchukue.”
“Kwani una haraka?”Aliuliza hans
Wala!? alijibu johari.
Ndipo kijana hans kwa swaga zake alianza kuomba maongezi kwa
Johari ili tu siku iishe kwani happy alikwisha mvuruga kwa kiasi kikubwaaa
“Basi tuendelee kuongea.”
“Wewe tu.” Alijubu johari
.
.
Kwa johari kuendelea kuongea kwake ilikuwa furaha kwa vile
muda mwingi amekuwa akishinda ndani tu huku akiwa mpwekeee na bosi wake huku akiwa boadi kwani
hakuweza kupiga stori na boss wake hata siku moja kwani alikuwa akieshimu kazi yake na kwavile aliweka heshima kwake mnooo.
Happy alipokuwa akienda kusuka na kutengeneza nywere zake alikuta
saluni imefungwa kwa siku hiyo huku kukionekana kuwa siku tofautiiii mno na
ndipo alipo shika simu yake na namba ya Irene,
Basi alipompigia simu Irene ambaye ndiye aliyekuwa ndiye mhusika
na mwenye saloon hiyo huku akipata majibu na alimwambia kuwa mwenye amepata
msiba na wasinge weza kufungua kwa siku hiyo. Happy alipo sikia hivyo nae
akatoa maamuzi ya hapo hapo na akaamua kugeuza gari na kurudi nyumbani huku
akiwa mnyongeee mno kwani alikuwa kapanga mipango mingi siku hiyo lakini
alipopokea hilo tu yote ilivurugikaaa mara moja.
Tukirudi upande wa pili kijana hans alionekana kunogesha
stori kwa Johari huku akimuuliza maswali magumuu mno mpaka kushinswa ongea.
“Halafu wewe utafanya kazi kwa watu hadi lini?” hans
alimuuliza johari ambaye alikuwa aking”atang”ata meno kwa aibu...
“Si mpaka Mungu atakaponijalia kutoka hapa na kuwa na maisha
yanguuu vipi kwani.”
“Kwani kutoka hapa mpaka Mungu akujalie?”
“Kwani we unataka kusemaje?”
“Mi nataka kukuoa.”
“He! Wee! Wewe unioe mimi, makubwa!” alijibu Johari huku
akichekaaa sana
“Kwani mimi nina nini?”
“Huna kitu na huna uwezo wa kunitoha hapa. Maisha yako
yenyewe ni hayo halafu ujiongezee mzigo wa mimi mmmmh huto weza hans?”
“Mimi nakumudu lakini mbona unanichukulia poa sana ipo siku
utanielewa tu”
“Hata kama.” Aliongea johari
Ghafla, wakiwa wanaendelea kuongea, mlio wa honi kutoka getini
gari la happu ulisikika. hans hakujua lakini Johari aliutambua mlio huo huku
akisimama na kuanza kutapa tapa na kutafuta kipi afanye, lakini happy huyo na
honi nyingine mfululizo na kuzidi kumpagawisha johari.
Lakini Johari alishindwa kuingia ndani, akabaki amesimama...
“Dada huyo,” alisema.
Hans anageuka tu, gari linakaribia geti...
“Dah! Noma sana,” alisema moyoni kijana huyo huku akijifanya
anaondoka zake...
“Yaani wewe bado upo tu hapa” johari una biashara gani na
huyu kibaka?” happy alimuuliza Johari kwa jaziba
“Sina.”
“Haiwezekani.”
Hans chukia sana kuitwa kibaka na happy
“Anti eee, mimi siyo kibaka bwana.”
“Kibaka wewe!” hans nae alionekana kuwa na hasira kwa kile
kitendo cha kuitwa kibaka na kutoa maneno ovyooo
“Johari ebu fungua geti tafadhali sana.”
johari alifungua geti, akazamisha gari na yeye akaingia na
kulifunga geti hilo kwa ndani. Moja kwa moja mpaka kwa mama yake happy lile
tukio aliloliona mda huo na kumuuliza maswali Johari na kukana aliona ni heri
afikishe kwa mama yake.
“Mama, huyu Maimuna mbona simuelewi”
“Kafanyaje?” mama alimuuliza happy
“Nimemkuta amesimama na kijana kibaka kibaka.”
“We johari? aliita mama mtu.
“Abee mama.”
“Ulisimama na nani, unataka kuniletea wezi hapa ndani siyo?”
“Mama siyo kibaka.”
“Ni nani?”
“Yule kijana anaye kuja kuchukua mabaki ya vyakula na
kupeleka kuuza.”
“Ha! Sasa na wewe happy, kwani humjui yule kijana?”
“Wewe mama unamjua?”
“Namjua sana, yeye ndiye anatupunguzia uchafu kuwa mwingi wa
kulipia. Si kibaka yule kijana sijawahi kusikia ameiba wala amefanya uhalifu
mahali.”
“Mh! Kwa hiyo we mama unamwamini siyo?”
“Bila wasiwasi?” Mimi sitaki kumwona hapa nyumbani na
akiendelea kuja kuna siku nitampiga risasi, nyie subirini tu.”
JE?
NINI KITATOKEA USIKOSE TENA SEHEMU INAYOFUTA
FOLLOW INSTAGRAM @storynzuri Update story nyingine
0 comments:
Post a Comment