BINTI NAMALA
SEHEMU
YA KWANZA
INTAGRAM @hanscharlz @storynzuri
Whatsapp +255652486818
.
.
Kilikuwa kipindi cha kiangazi katika kijiji cha
SOWETO, ilikuwa ni majira ya jioni bwana TUMBAKU alikuwa akirudi zake nyumbani
kwenda kumalizia siku, alikuwa akitokea shambani naye kuipita mahala ili
ashushe kiu yake aliokuwa katoka nayo shambani naye alipita mahara na kuanza
kufanya yake, alikunywa mpaka kuzikinai na huku akiona mda ukizidi kwenda
aliaga lakini vijana wenzake walikuwa bado wakimwitaji kwani alikuwa na vionjo
pindi walipokuwa wakipata moja moto moja baridi huku akionekana kuwa
mtubwizaji……
“haaaaaa! Unataka kuondoka mapaema yote hiii”
ilisikika sauti ya kijana mwenzake ikiongea
“ndio kwani nyumbani kwangu mlango uko wazi”
“hakuna wezi kijijini kwetu bwana twendeleee kidogo”
“nusu saaa tu inanitosha………Mama ngeza nyingine hapa”
Waliendelea kupata dozi ya nusu saa huku bwana TUMBAKU
akiwa makini sana kuofia kuzidisha kiwango cha kunywa kwa siku hiyo basin aye
alikuwa akinywa kwa speed ya chini huku akiona wenzake wote wako chapaka chapa
hoi……….
.
Ilifika wakati aliona ni bora ajinyanyue ili aanze
safari kurudi kwake kwani kulikuwa na mwendo kutoka pale, basi aliwachomoka na
kubeba chupa moja na kuzunguka nyuma ya nyumba ile na kutokomea polini naye
alipoipata barabara alianza kutembea huku akiimba ovyo ovyo barabarani….. sauti
ile ilikuwa ikisikika kwa wingi wa ukinya kwani kijiji kilikuwa kimetulia mno
huku wanakijiji wote walikuwa kwenye majimba yao wamelala.
Bwana TUMBAKU alijawa na wasiwasi kuhusu mlango wake
huku akiwaza huwenda vibaka wameshapisha lokoo kwenye nyumba yake basi alizidi
kuwai huku akienda akipiga mafundo mdogo madogo njiani, ilifika mahari aliona
potelea pote kwani mda ulikuwa ushakwenda naye ilimbidi aanze kwenda mdogo
mdogo……., alifika mahari ndege waliaruka kwa fujo na walimtia wasi wasi sana
huku akili zake zilirudi naye kushika siraha yake na kutazama kwa umakini sana
pande zote naye kusikia vishindo vijija kwa kasi aliwaza ni nini kile naye
alikaza siraha yake mkononi na kujiandaa na mapambano.
Vishindo vile vilimfanya kujirudi kiakili naye ndipo
alipojificha kwa pembeni na kukitazama kishindo kile na kuona ni kitu cha
kawaida tu alijizarau
Na kuendelea na safari zake, lakini alipokuwa akizidi
kupiga hatu aliona kitu kwa mbele yake kilicho mtia wasi wasi lakini aliona ni
kama cha mwazo basi alitamba barabarani, lakini kadri alivyo kuwa akikisogelea
aliona ni cha utofauti wa hali ya juuu naye ndipo alipoona mtu akiwa juu ya
farasi nae akija kwa sipidi iliomuogopesha bwana TUMBAKU na kutaka kujificha
lakini alishindwa pale alipomwona msichana ndiye anaye ongoza ile farasi….
Bwana TUMBAKU alishika siraa yake huku akirudi nyuma
nyuma akisogea maeneo mazuri, lakini wakati alipokuwa akirudi nyuma alijikwaa
kwenye jiwe naye kudondoka chini lakini bwana TUMBAKU alikuwa shupavu naye
alinyanyuka haraka na kuangalia usawa wa kukimbia naye alitoka
ndukiiiiiii………….. mpaka mahara pasipo na msaada basi binti yule aliyejulikana
kwa jina la NAMALA alipoona kile kitendo cha bwana TUMBAKU kukimbia kilimfanya
kuwa na wasiwasi “kwanini alikimbia” alijiuliza na mwisho wa yote alimwamulu
yule farasi kwa viboko huku akimwongoza njia naye kumfatisha mahara alipokuwa
akikimbilia…..
.
.
Bwana TUMBAKU aliishiwa na nguvu za kukimbia huku
akibaki ameshika magoti yake na kutazama mahali pa zuri ili ajifiche kwani aliona
binti yule kwa kumwangalia alikuwa ni hatari. Licha ya kuwaza vile bwana
TUMBAKU alipata mahara pa kujificha naye kuingia vizuri na kutokomea kwenye
upenyo uliokuwa ni mkubwa kwake.
Binti NAMALA alizidi kuzifuata nyayo za Bwana TUMBAKU
mpaka hapo alipoona hana mwelekeo wa kumwona bwana TUMBAKU naye alibaki
akijiuliza yuko wapi lakini kwa uwezo aliokuwa nao binti huyo hakuweza kuishia
pale naye alizidi kuzikata mbuga na kuzidi kumfata na kunusa harufu za bwana
TUMBAKU. Alifika mahali binti NAMALA aliona nyayo za yule mtu aliye kuwa
akikimbia naye si mwingine ni Bwana TUMBAKU zikiishia kwenye kichaka naye kuona
vile alijua mahali pale kuna njia ya chini chini ambayo ilikuwa ikitoka upande
wapili basi alimgeuza farasi wake na kuelekea mahali palipokuwa na njia ile……
aliwai na ndipo alipokuwa kabaki akimgoja naye aweze kutokeza ili amkamate
vizuri bwana TUMBAKU….. licha ya bwana TUMBAKU alikuwa kwenye akipita kwenye
vichochoro vile wala alikuwa
Hajui mahali alipokuwa akienda naye ndipo alipoona
mwanga na kujua kaishafika upande wa pili aliwai na kufika naye alipo toa kichwa
chake alishanga sana kuona… sura ya binti NAMALA ikimwangalia kwa hasira kali
na iliompekea kudondoka mwenyewe lakini alijitaidi na kunyanyuka mahali pale na
kutaka kurudi tena ndani ya ule uchochoro…..
Bwana TUMBAKU hakuweza kurudi kwani dhoruba alizopata mle
ndani zilikuwa sio za kitoto basin ae kuangalia upenyo mwingine na kukimbia. Na
ndipo iliposikika sauti ya binti NAMALA ikimwita bwana TUMBAKU….
“wewe kijana simama hapo mara moja nakuambia…………?”
.
Bwana TUMBAKU alishitushwa sana na sauti ya Binti
NAMALA ilipokuwa ikisikika huku naye akizidi kupepea kwa mwendo wa feni huku
akipishana na upepo na kuacha vumbi nyuma…
NAMALA alimwelekeza farasi wake nae kuanza kumfata kwa
kasi iliompelekea Bwana TUMBAKU alipokuwa akimwangalia nyuma binti yule aliona
akizidi kumsogelea kwa kasi ya hatari…… ndipo alipokuwa akizidi kugeuka nyuma
aliruka hatua mbili na kujikwaa chini na kudondoka chini na ndipo hazikupita
hata sekunde nae binti NAMALA alifika eneo la tkio na kumkuta yuko chini na
kuanza kumzunguka huku akimchanganya Bwana TUMBAKU mahali alipokuwa
kadondokea….
Bwana TUMBAKU hakuwa na ujanja wowote wakati ule naye
alisubilia tu kile atakachofanya binti NAMALA huku naye akipumua haraka haraka
na mapigo a moyo wake yakimwenda mbio huku akijua ndio mwisho wake basi naye
alibaki akitizama kile alichokuwa akifanya binti NAMALA
.
.
Binti NAMALA alicheka kwa kicheko cha zarau huku
akimwangalia sana Bwana TUMBAKU…
“hahahahhahahhahaaaaaa kijana msitu huu tunaujua sisi”
alicheka na kumalizia na manen ambayo yalimfanya bwana TUMBAKU kujijua kuwa
ndio umefika mwisho wake lakini cha kushangaza alimwona Binti NAMALA akiinama
na kutoa kitu ambacho kilimfanya kujiuliza kwa mara nyingi nyingi anataka
kufanya nini ili aweze kukizuia kwa uwezo wa kuokoa maisha yake naye Binti
NAMALA alishika……………..”
.
Naye bwana TUMBAKU alishindwa kuzizuia mbini za binti
NAMALA pale alipo msogelea na
Kumweka kwenye mikono yake huku binti huyo alikuwa akicheka
pindi alipokuwa akimtizama bwana TUMBAKU huku akinena kwa mdomo wake
“bwana hapa ndio umefika kwa binti katiri kuliko
mabinti wote humu porini”
Bwana TUMBAKU alitoa macho na kubaki akimwangalia sana
binti NAMALA kwa kile alichokuwa akikiongea naye ndipo alioona ni vyema kutumia
njia ya pili…. Kwa kutaka kushika siraha yake, lakini hakuweza kwani binti
alikuwa kaishamwona muda mrefu sana huku binti huyo alingoja tu afanye kile
kitendo naye amwingilia vizuri.
“unataka nini kwangu binti?” Bwana TUMBAKU aliuliza
huku akionesha sura ya unyonge kwa binti aliyeonekana kuwa na majigambo
makali..
“hahahhhahahahha”
Binti NAMALA alicheka kicheko kilichomshitua tena Bwana TUMBAKU
“mbona unacheka hivyo kulikoni?”
“basi tu nakuurumia hapa”
“kwa kipi tena binti”
“unavyoonekana tub ado sana uwezo wa kuniponyoka mimi”
“haaaaaaah hilo ndilo limekufurahisha”
Bwana TUMBAKU aliongea naye kutizama kwa pembeni
aliona binti kaifazi chupa lenye maji naye ndipo alipoona si budi kumwacha
kumwomba japo atulize kiu aliokuwa nayo….
“samaani dada…….”
“bila samahani” aliitika Binti NAMALA huku akionekana
kuwa makini sana
“nisaidie japo fundo moja la maji yako”
Ilimchukua takiribani dakika kazaa mpaka alipopata
nini afanye naye alionekana mdogo mdogo akigeuza shingo yake ili aweze
kumsaidia Bwana TUMBAKU……
“sawa haya hapa”
USIKOSE SEHEMU INAYO FATA HAPA HAPA
0 comments:
Post a Comment