Logo Design by FlamingText.com
Logo Design by FlamingText.com

storynzuri UTAMU WA TUNDA sehemu ya kumi na tisa


.
.
UTAMU WA TUNDA SEHEMU YA 19
MTUNZI HANSCHARLZ
INSTAGRAM @hanscharlz @storynzuri
Whtsapp +255 652486818 kwa 5000# tu.
.                         
Ilipishia
Baba alichomoka na kwenda sebuleni na alipofika alimwoana Happy kakaaa akiangalia video naye moja kwa moja mpaka alipokuwa kakaaaaaa…..!
.
“We? Happy kulikoni utaki kile mama alichokuambia” baba alifika bila ya kutaka salaamu wala nini alifikia kwa swali na kumfanya mtoto wake Happy amtizame huku akifikilia kutoa jibu
“Baba mimi kwa sasa sitaki kuolewaaa!” Happy alijibu huku akimsogelea baba yake kwenye miguu yake.
“sasa mwanangu uoni kama umekuwa”
“naona baba lakini sijajipanga kwa hilo dady…………..!”
“duuuuuh! Ni wewe au kuna mwingine anakujibia hayo majibu?”
“no dady ni mimi mbona”
“umebadilika mwanangu au ni yule kijana”
“daday………..!!” Happy aliongea maneno yale ya mwisho na kupenya mpaka mbali mno na kumfanya ashike kichwa chake na kuondoka enei la sebuleni,
Baba alishangaa sana kumwona binti yake akimwacha na kukimbia chumbani mwake na kuufunga mlango wake kwa nguvu, na kuonekana kukelwa kwa kile alichokuwa akiongea naye.
Happy kwa asila zile zilimfanya ajitupe kitandani na kuukumbatia mto wake na kuwaza sana juu ya kile walichokuwa wakimwambia kuolewa wakati yeye sasa yuko na mimba tena ya mtu yule aliokuwa akimpenda sana, alipitiwa na usingizi mkali uliompa ndoto za ajabu na vitisho huku akishituka shituka mara kwa mara lakini mpaka kulipo kucha, naye kulipokucha tu aliamka kitandani na kunyata kwenda kwa kijana Hans naye alifanikiwa kutoloka nyumbani hapo na kuelekea Getoni mwa kijana Hans naye alipofika kama alivyo zoea alisukuma mlango na kuingia ndani, na kumkuta kijana Hans akiwa kwenye pozi la usingizi basi ndiye aliyekuwa wa kwanza kumwamsha huku akimpa busu zito lililo mfanya kushituka huku akiendelea kula denda na ndipo alipofumbua macho na kumwona binti Happy na kutoa tabasamu zuri.
“vipi za kuamka mpenzi” aliuliza binti Happy
“niko poa Happy wanguuuuu!” alijibu Hans huku akimpapasa kwenye mkogo na kumfanya kuwa mtoto mdogo kwenye mikono yake, basin aye Happy alikuwa mpole pindi kijana Hans akiwa kwenye kitengo chake
“Hans……..” aliita binti Happy
“yes Happy….!
“nakupenda sana tunza pendo langu nalo kupaaaa”
“nakupenda Happy pia lakini wafahamu fika kuwa wazazi wako wananiona kama taka taka ujue?”
“yah!!! najua lakini mimi ndiye naye chagua wala sio wao hilo mpenzi lisikupe shidaaa sawa”
“sawa mpenzi” Hans alijibu huku akiwa kifuani mwa binti Happy akipata joto la asubui
Walikwisha kuongea naye kijana Hans alipo mtaka binti Happy arudi kwao lakini cha kushangaza kwa kijana Hans kumwona binti akikataaaa kurudi kwao,
“Happy mpenzi sasa itakubidi urudi nyumbani name niendee kwenye mizunguko kutafuta japo pesa kidogo siunajua tena”
“we nenda utanikuta hapa hapa” alijibu huku akivuta shuka kujikunyata kwenye kitanda cha kijana Hans
“mmmmmm! Sawa” alijibu kwa kinyonge naye kuondoka kwenda kwenye miangaiko yake
.
.
Kulipokucha chumbani mwa baba na mama Happy kulikuwa kumepamba moto kwa maada ya mwanao huku mmoja akiwa upande wa mtoto na mwingine kuolewa
“mama Happy mtoto huyu itabidi aolewe tu kwa namna yoyote ile na mtoto wa rafiki yanguu na leo wanakuja nyumbani hapa”
“baba happy mbona mapema sana kwa hili jambo”
“mama happy bwana mtoto sasa kawa mjanja na tukikaaa hivi hivi atakuwa sugu ni bora kumpatia kijana mapema”
“mimi kwa hilo bado ujanishawishi mme wangu”
“kwanini mimi nataaka mtoto aolewena si vingine” baba aliongea na kumwachia mama Happy fumbo ambalo alibaki akijiuliza juuu ya kile baba Happy alichokuwa kaamua, basin aye alijisemea moyoni “mmmmmh mtoto wangu jamani, lakini nitapambana”
Mama alitoka moja kwa moja mpaka chumbani kwa mtoto wake lakini hakuweza kumkuta na kumuita kijakazi Johari,
“Johariiii Johari Johariiiiiiiiiiiii!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!” mama aliita kwa sauti kubwa huku akifikilia kuwa Johari naye hakuwepo basi alisikia kwa mbali sauti ikiitika,
“abeeeeee!!!!! Mama”
“Happy yuko wapi?” mama aliuliza
“sijui mama”
“ujui inamaana hakukuaga hata akitoka”
“mmmmh mama sikuizi Johari kabadilika hata kuniaga huwa afanyi hivyo na wala leo ajaniaga”
“atakuwa kaelekea wapi?” mama alimuuliza tena Johari
“mmmmmh labda kwa kijana yule mchafu?
“toka lini au ndio mchezo wake sikuizi”
“mama hapo mimi sielewi sijajua kama kaenda huko”
“okay sawa kwa huyo kijana unakujua vizuri”
“sikujii vizuri lakini njia nyepesi ni kuulizia tu kwani kijana huyo anajulikana sana mtaani hapa”
“eti heee basi sawa twende”
.
.
Mama pamoja na Johari waliongozana kuelekea kumtafuta Happy huku wakianza kwa kijana Hans, basi walipo ingia changanyikeni kidogo (uswailini) walikutana na vijana wawili waliokuwa wakipiga stori vijiweni naye mama aliwasogelea ilia pate kuwauliza
“vijana samahani”
“bila samaani mama”
“haaaaa! Nilikuwa na mtafuta kijana mmoja yle mchafu anaye pita kila nyumba uwenda mnapafahamu kwao”
Vijana wale bila ya kufahamu ili wala lile walijikuta wakilopoka sana na kumfanya mama Happy kupata mwanga wa kwenda kwa kijana Hans
“haaaa yule aishi kwao yule kapaga kwenye geto moja hapo kati bimkubwa”
“maeneo yapi?”
“unaona pale kwenye mti mkubwa”
“yah napaona mwanangu”
“basi ndio hapo bimkubwaaaaa”
“asanteni” naye mama Happy alipokwisha kuelekezwa alianza kupiga hatua lakini vijana walimwita
“bimkubwa vipi sasa hata ya maji tuangalie na sisi basi”
“hoooooh shikeni hiyaapa wanangu”
Basi mama Happy aiwapa naye kuondoka kuelekea pale alipo ambiwa na vijana hao basi alifika mpaka mlangoni alipokuwa kaelekezwa na vijana wale na kugonga mlango.
Happy alishituka mtu akigonga mlango naye ilimbidi atupe shuka pembeni ili aweze kwenda kuufungua mlango naye alipofika mlangoni aligungua mlango ule……”


JE NI NINI KITAENDELEA KWA BINTI HAPPY ALIPOUFUNGUA MLANGO ULE? 
Share on Google Plus

About storynzuri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment