.
.
UTAMU WA TUNDA SEHEMU YA 22
MTUNZI HANSCHARLZ
INSTAGRAM @hanscharlz @storynzuri
Whtsapp +255 652486818 kwa 5000# tu.
.
Ilipishia
.
“nakwambia lakini mimi ni
kijana nakupenda Happy mno”
“kweli nami pia Hans”
Happy alijibu huku akitabasamu na kuzidi kuchanganyikiwa huku mawazo yake yote
akiwaza ndiye mume sahihi atakaye kuja kumuoa na siyo Clinton…….?
.
Hans alimpapasa papasa
maeneo flani mwa binti Happy huku akimfanya kuwa na Amani na furaha wakati
akiwa naye, kweli kijana Hans alikuwa fundi wa mapenzi kwani alipoanza
kuzichezea chezea nywere za binti Happy huku akiupandisha mkono wake na
kuushusha mpaka kona zote za kichwa cha binti Happy, Happy alizidiwa na
kujisikia raha kichwani mwake na kumpelekea kulala usingizi kwenye mapaja ya
kijana Hans, aliuchapa usingizi mapajani mwa kijana Hans na kumpelekea kijana
huyo kushindwa kwenda kwenye mizunguko yake aliokuwa kapangaaa kwani ilimbidi
ampeti peti na kumpa masham! sham! Ambayo alijua fika hato chomoka kwenda kwa
kijana yoyote bali ni yeye tu.
Ugovi ulizuka mama pamoja
na Baba Happy juu ya kukimbia kwa mwanao Happy mahali pasipojilikana huku
ikionekana kuwa baba ndiye msababishi…………….!
“umefanya nini mume
wangu?” mama Happy aliuliza huku akimsogelea mumeweeee
“mama Happy mbona
sijafanya chochote kile licha ya kile nilichokuambia tu juuu ya Clinton na
Happy wetu” baba alijitetea kwa mama Happy
“hapana mbona mtoto ka
toka mbio hivyooooo?”
“huwenda kile nilichokuwa
namweleza ndicho kimemchafua”
“tunampata wapi sasa
maana hapa kaishatokomea”
“natoka sasa kwenda
kumtafuta”
.
.
Baba Happy alipokwisha
kuongea naye alianza kupiga hatua kwuelekea nje ili achukue gari ili akamtafute
binti yao, lakini wakati akizikaribia kuta za mlango alisikia sauti ya mama
Happy ikimwita.
“mumewanguuuuuu”
“yes sweet”
“ebu ludi na wazo hapa”
baba Happy alirudi na kuitika wito wa mama Happy naye kumfata alipo, na
kumsikiliza.
“nimekuita mume wangu
unaonaje tukimpata Happy tumrudishe kwa UINGEREZA aendelee na masomo yake”
“mmmmmmh na Clinton je? Baba
aliuliza kwa mshangao
“mtoto ataki kuolewa na Clinton
au ujamwelewa”
“siyo kwamba hivyo mama
Happy”
“ilaaaaaa!!!”
“ngoja kwanza nikamtafute
nikirudi tutaongea vizuri mke wangu”
“sawaaaaaa!” mama
aliitikia bila y ahata kumwelekeza mahala atakapo mpata binti yao
Baba happy alichomoka
ndani na kwenda kumtafuta Happy nae alipita kila kichochoro alichokuwa akijua
kuwa Happy uwenda atakuwa maeneo yale ila wapi alibaki kuchoma mafuta yake na
kumkosa mtoto mpaka jioni aliporudi nyumbani, aligonga mlango na kufunguliwa
naye aliye mfungulia mlango ule alikuwa ni Happy mwenyewe, baba alishituka
kuona sura ya mwanae mlangoni.
“wewe ulikuwa wapi”
“kwa rafiki yangu? Happy
alijibu kwa madoido huku akiuiga mguuu wake chini
“mbona nimezunguka kote
sikukuona”
“dady nilikuwa kwa rafiki
yangu”
“sawaaaa”
.
.
Baba aliingia ndani na
kwenda moja kwa moja mpaka chumbani mwake na ndipo alipo mwanzishia mke wake
tifuuuu ambalo lilichukua mda kidogo kumalizika kwani baba Happy alionekana kutopenda
kile kwa mwanane na kuamini ya kuwa mama yake ndio atakaye kuwa anahusika kwa
kila alichokuwa akikifanya Happy.
Zilipita wiki nne huku
Harusi ya kijana Clinton pamoja na Happy ikipamba moto huku wana harusi hao
hakuna hata moja aliekuwa akiwa na mazoea yam da mrefu na mwenzake licha ya
kukutanisha mara kazaa huku mda mwingi kijana Clinton alikuwa akiutumia
kutembea nab inti Happy huku akiwa hafahamu chochote juuu ya binti Happy, Clinton
aliona siku zikizidi kuchelewa naye alimwomba binti Happy siku moja watoke huku
naye Happy hakuwa na uwezo wa kukata ilibidi ampange siku ili waweze kukutana. Nao
walipanga na siku ilipowadia wote wawili hao walikutana mahala faraga nje
kidogo na kwao huku Happy mimba ikizidi kushika kasi licha haikuwa ikionekana
sana naye alikuwa akivaa nguo zilizokuwa zikiendana na hali yake.
“oooohoooooo! Happy
nimefurahi kwa wito wangu kuutekeleza” aliongea Clinton huku akimtizama mtoto
mzuri Happy
“nami pia ahsante kwa
kunireta mahara hapa”
“lengo nililokuitia Happy
ni kuhusu swala langu kwako natumaini kila kitu wakijua”
“Clinton najua lakini?”
“lakini nini Happy”
“mimi siwezi Clinton kuolewa
sasa”
“Happy ukisema hivyo
wakosea na ndoa imepangwa wiki hiii uoni utakuwa umenikosea mimi pamoja na
wazazi wako kwa ujumla”
“kweli Clinton” alijibu
Happy huku akiunganisha na fundo la juisi ilikuwa mezani mwake
“fikiria sana Happy
napenda tuwe pamoja nawe kwani nimependezwa nae uwe mke wangu”
Happy alishindwa kujibu
naye alionekana kwa muoga kwani hakupenda kumsaliti mpenzi wake Hans, naye
ilimbidi aombe kuondoka ili awai nyumbani kwani mda waliokuwa wamekutana
ulikuwa umekwenda mno, basi naye alichomoka na kurudi nyumbani na alipofika
nyumbani alikuta watu wakiwa sebureni wakizungumza naye alipitiliza moja kwa
moja mpaka chumbani mwake.
Happy alifika chumbani na
kuwaza sana huku akihesabu siku zilizokuwa zimebaki na kuona ni chache kwake
kufanya uamuzi aliokuwa akiuona ni uamzi mgumu, ilimbidi apumzike kuondoa
mawazo yote ya siku nzima naye kupitiwa na usingizi na aliposhituka tu kulikuwa
kumekucha naye alichomoka asubuhi hiyo na kwenda kwa kijana Hans naye alikuwa
kajilaza kwa shughuri ya siku iliopita ilionekana kuwa ngumu kwake naye binti
Happy alipitiliza mpaka getoni mwa kijana Hans.
“baby…..!” aliita binti Happy naye kijana Hans
kuchungulia kwenye shuka na kumwona ni mpenzi wake
“happy baby!”
“mbona mpaka sasa uko
kwenye shuka kurikoni”
“uchovu tu Happy”
Happy aliona kuwa ni
vyema kupanda juu ya kitanda ili amfanyie masaage kidogo ili kumuweka kuwa
fiti, alianza kumminya minya kwenye mgongo wake…….!
“umejuaje kama naitaji
vitu kama hivyoooo!”
“mmmmmh Hans bwana
unanifanya sijui mtu akiwa kwenye hali kama yako huitaji nini”
“sawa ndiyo najua leo
baby”
“hahahahhahaha sawa”
alicheka na kumminya sehemu ambayo kijana Hans alipata raha huku akimwambia
“hapo hapo Happy”
JE NI NINI KINAENDELEA
USIKOSE SEHEMU IJAYO?
0 comments:
Post a Comment