.
.
UTAMU WA TUNDA SEHEMU YA 21
MTUNZI HANSCHARLZ
INSTAGRAM @hanscharlz @storynzuri
Whtsapp +255 652486818 kwa 5000# tu.
.
Ilipishia
.
Mama alikwisha kuongea
yale naye kumkaribisha kijana ili aingie chumbani mwa binti Happy naye aliingia
na ndipo alipo mtazama Happy kijana yule moyo wake ulikwenda mbio sana….?, na
kumsogelea kwa ukalibu binti Happy huku naye Happy alipomwona kijana Yule wala
hakuwa na raha yoyote ile ila alitaka kumfurahisha nafsi yake tu.
.
“mambo Happy!”
“poa” aliitika kwa
kinyonge binti Happy huku akimtizama kijana yule ambaye hakuwai hata siku moja
kumwona licha ya kuwa akisikia tu taharifa zake kipindi yuko masomoni naye,
“naitwa Clinton”
“nafurahi kukujua Clinton”
alijibu huku akitizama chini binti Happy
“okay sawa Happy
natumaini tutajuana vizuri” Clinton aliongea huku akimwachia tabasamu kali
binti Happy naye kutoka chumbani mwa Happy na kurudi tena sebureni alipokuwa
kamwacha baba yake pamoja na wazazi wake Happy.
Alifika sebureni na kukaa
pembeni ya baba yake na kusonya naye kidogo huku akimsifia kuwa kamchagulia
msichana mzuri
“daaaaaah! Dady Happy
kweli Happy kweli name nimeridhia kuwa naye binti huyu”
“mmmmmmm! Kweli mwanangu!”
“yah! Dady”
Basi mama Happy pamoja na
Baba Happy walikuwa wakimtizama Baba yake Clinton pamoja na mtoto wake wakiwa
kwenye hali iliokuwa ikiwalidhisha kwani walipokuwa wakinong’onezana tabasamu
kwa mbali kuonesha kuwa Clinton kampenda binti yao licha ya kumwona siku ya
kwanza basi wazazi wake Happy walishikana mikono huku baba mtu akiwa kwenye
tabasamu kali na mama naye huku akiwa hana furaha yoyote ile kwani alikuwa
akijua kuwa binti yake anamimba ya kijana Hans, ndipo Baba yake Clinton alipoona
mda wake wa kuwa pale umefika tamati ilimbidi ajiongeze kuaga familia ya binti
Happy ili wakajipange vizuri kuja kumchukua binti Happy ili akaishi na mwanae Clinton.
“haaaaa! Mzee mwenzangu
mimi mda umenitupa mkono kuna mahali nahitajika tutazidi kupanga na kufanikisha
zoezi hili”
“okay sawa mzee mwenzangu
name sitakutupa mkono tutalifanikisha”
Walishikana mikono wawili
hao na kuondoka kwa baba yake Clinton, Baba Happy alimtoa mzee mwenzake na
aliporudi ndani mama Happy alikuwa akimsubilia kwa hamu sana sebureni ili
kufunguka kwa kile kilichokuwa kikiendelea nyumba ya pazia kwa binti yake.
“mumewangu mwanao kama
unavyo msikia kukubali kwa hili unalo taka kufanya kwa sasa”
“mkewangu acha fikira
hizo siku zote nakuambia mimi ni kichwa cha familia Happy atakubali tu?
“mmmmmm!” ulisikika mguno
wa mama Happy pembeni na kubaki akijisemea mwenyewe juuu ya jambo hilo
.
.
Happy alibaki chumbani
akiwaza nini afanye juuu ya kile baba yake anachotaka kumlazimisha kufanya huku
moyoni mwake hakukuwa na makubaliano ya kitu hicho, aliwaza sana huku
akibadilisha mapozi kitandani mwake na ndipo alipoona njia sahihi ni mama yake
naye alitoka chumbani mwake na kuelekea sebureni na kumkuta mama kashika kichwa
huku akiwaza sana naye taratibu alijisogeza mpaka pembezoni kidogo kwa mama
yake alipokuwa kaka naye kumshika kwa nyuma, mama alishituka sana.
“we Happy kulikoni”
“hamna mama nimekuja tu
nakuona uko na mawazo mengi”
“ungejua mwanangu hapa
nakufikilia wewe tu”
“mama mimi tena!!!!!!
nini hicho”
“kuolewa mwanangu na
kijana Clinton baba yako yuko na msimamo wa hali ya juu”
“mama mimi kuolewa
naolewa lakini siyo kwa mtu ambaye sijapanga kuolewa naye”
Mama happy alishika
kichwa chake aliposikia yale maneno yaliokuwa yakitoka kinywani mwa binti yake
na kumfanya kuchanganyikiwa Zaidi, na ndipo mama alipo nyanyuka mahali
alipokuwa kaketi na kusimama.
“mwanangu unasemaaaa nini
au sijakueewa?”
“mama mimi sitoolewa na mtu ambaye sijapanga kuolewa naye” Happy alijibu huku akiwa na msisitizo
“mama mimi sitoolewa na mtu ambaye sijapanga kuolewa naye” Happy alijibu huku akiwa na msisitizo
“mwanangu kaa chini na
fikiria sana kauli zako hii bahati mwanangu”
“mama mapenzi si pesa……………..!!!!”
Happy alimalizia kusema vile na kurudi chumbani mwake kuendelea kuuguza kidonda
chake cha kufikilia ni jinsi gani wataweza kufanikisha kumwelewa kijana Hans na
siyo Clinton.
Mama alimwangalia mwanae
Happy akiondoka huku akiwa na msimamo wake ule ule huku ukimfanya
kuchanganyikiwa Zaidi naye kujitupa kwenye sofa lililopo karibu na kupitiwa na
usingizi uliochukua takiribani nusu saa, alishituliwa na mumeweee naye kuinuka
na kukaa vizuri.
“Happy yuko wapi” Baba
Happy aliuliza
“yuko chumbani mwake”
“okay sawa ngoja
nikazungumuze nae”
.
.
Baba Happy alizungumza na
kuanza kuufuata mlango wa binti yake na alipofika aligonga mlango naye baba
kuingia ndani.
“Happy!!!!!!!!!!!!!!!!”
“yes dady” aliitika binti
Happy
“umeona mambo yameiva
mwanangu usiniaibishe kwa rafiki yangu”
“Babaaaaaaaaaaaaaaa?”
“nini”
“nimekwisha kukueleza
hali yote”
“usitake kuniambia kuhusu
yule kijana mimi nilimuruhusu akukate kiu yako tu na siyo vinginevyo”
“ukisema hivyo baba
unakosea”
“nakosea nini basi sasa
mimi ndio baba yako na nimeshapitisha Clinton akuoe”
“Baba hunipi haki yangu
kama mtoto wako” Happy alizungumza maneno yale na yalimfanya baba yake kumwacha
hoi huku akifikilia ni kweli ila atafanya nini na ni rafiki yake.
Happy alichomoka chumbani
na kumwacha baba yake akiwa ajielewi naye kupita sebureni mkuku huku speed ile
ilimchanganya sana mama yake nae mama kumwita akini Happy hakuweza kugeuka,
baada yam da mfupi Mama Happy alimwona mumewe naye akitoka kwa speed na alipofika
sebureni tu
“mke wangu Happy kapita
hapa?”
“ndiyo tena kwa speed
kali sana kulikoni”
“mtoto kaishakuwa ana
akili sasa duuuuuuh!!!!” Baba alijibu huku akimwangalia nje ya geti, naye
hakuweza kumwona.
Happy alitokomea mpaka
kwa kijana Hans na alipofika getoni mwa kijana Hans aliweza kumkuta akiwa
anataka kutoka kwenda kwenye mizunguko yake ya kila siku naye kijana Hans alipo
mwona mpenzi wake Happy alisitisha kile alichokuwa akifanya nan a kuingia naye
getoni.
“mpenzi wangu!!!!!!” aliita
binti Happy
“yes baby”
“vipi ujaenda tu kwenye
shughuri zako”
“yah ndio nilikuwa
najiandaaa mpenzi”
“Okay vizuri lakini
mpenzi?” alisita kuongea alipokwisha kuongea kitu kile
“lakini nini”
“familia yangu mpenzi”
“nilikuambia Happy wazazi
wako hawapendi kuniona sasa na ninavyo mwogopa mama yako si atanipeleka segerea
mimi”
“usifikilie hivyo Hans”
“nakwambia lakini mimi ni
kijana nakupenda Happy mno”
“kweli nami pia Hans”
Happy alijibu huku akitabasamu na kuzidi kuchanganyikiwa huku mawazo yake yote
akiwaza ndiye mume sahihi atakaye kuja kumuoa na siyo Clinton…….?
.
JE NI NINI KITAENDELEA
USIKOSE SEHEMU INAYO FUHATA HAPA HAPA KUNDINI
NIPO WEEK YA TEST CHUO SO
NITAKUWA NACHELESHA SANA STORY
duuu mapenzi si pesa
ReplyDelete