Logo Design by FlamingText.com
Logo Design by FlamingText.com

storynzuri sehemu ya sitini shemeji ingiza pole pole


.
.
.Sehemu ya sitini

Mtunzi INSTAGRAM @hanscharlz @storynzuri 
.
Ilipoishia "Nani nilizidi kumwomba msamahaa dada amina lakini nae alianza kulia tu huku akiishiwa nguvu huku akikosa maneno kwani nae aliangua kilio huku nami pia nikiangua kilio hicho.
Na ndipo dada amina alinyanyuka na kuniangalia sana huku mimi nikiona aibu sana kwa kile nilichofanya nami niliona chochote atakacho hamua kwangu sawa nae alinyayua mdomo wake na kuanza kuniambia?
.
.
"Isabela isabela wewe wakunifanyia hivi dada yako siamini" alijawa na mtetemo ndani ya mdomo wake na kushindwa kuongea tena na kukimbia chumbani mwake huku akilia. 
Nilibaki nikiwa sina Amani kwa kile alichokuwa kaonesha dada amina kwa kunikimbia huku nikifikilia ya kuwa huwenda dada amina ataki kuniona tena au vipi nilibaki nikijiuliza sana kwa kile nilicho jionea lakini nilivuta subira na kujisemea moyoni "huwenda ni hasira" 
shem Erinest alikuja na kuninyanyua mahari nilipokuwa nimedondokaaa na ndipo nilipo nyanyuka.
"Isabelaaaa kulikoni tena wala usijali atakusamehee tu okay" Erinest aliongea na kunipa moyo
"mmmmh kweli maana naogopa sasa akitoka ndani itakuwaje" nilimjibu huku nikiwa naagalia mlango wa dada amina endapo akitoka nimuone maana anaweza kutoa uhai wangu niliofia hicho
"wala Isabela usiogope kwani ni vyema umekuja na kuliko kutokuja"
Nilibaki nikiwa nawaza tu dada amina pale atakapo toka ndani nitakuwa vipi endapo akija na kitu cha kunidhuru. sikuwaza sana nae alitoka chumbani na nilipo mwona tu moyooo wangu ulishituka sana kumwona mkono wake uko nyuma huku akija mahari nilipo huku akiniangalia sana na alipofika na kulitaja jina langu "ISABELAAAAAA!!!!!!!!"
nilishituka sana na kubaki nikiwa kimya huku nikimtizama nae aliongea huku mimi nikiwa natetemeka sana kwani nilipatwa na mtetemo mahari nilipo huku nikitega sikio langu kwake
"Isabela nimeumia sana kwa kile ulicho fanya kwa mpenzi wangu na huku ukijua fika  hasa navyo mpenda  mnoo!! Erinest lakini hakuna jinsi wewe bado utakuwa mdogo wangu"
niliendelea kumsikiliza huku nikiwa makini sana maana dada amina hubadilika ndani ya dakika 1 ya maeongezi nae aliendelea 
"Sina budi kuweka chuki kati yangu na wewe kwani inauma lakini moyo wangu kwako uko mweupe kwani umejua kosa lako na kuja kuniomba msamahaa basi nami nimekusameheeee Isabela"
Alipo kwisha kusema neno la mwisho nami nilibadilika na kuwa na furaha na kunyanyuka mahari nilipo na kumfata na kumkumbatia huku nikitwokwa na machozi na kumwmbia 
"Asante sana dada kwani alikuwa ni shetani alinipitia kufanya upuuzi huo basi nami sito fanya tena hivyoooo"
"sawa Isabelaaaaa!!!!"
.
.
Nilikuwa mwingi wa furaha huku nikiamini kuwa sasa niko free kuwa na Erick mda na mahari popote bila kuwa na buguza au usumbufu hulio kuwa ukipelekea kuwa na hofu na wasiwasi pindi nimuonapo Amina na shem Erinest.
Basi dada Amina aliingia chumbani mwake huku akiniacha sebureni mimi pamoja na Erinest na ndipo Erinest aliponisogerea karibu yangu huku nikiisi kuwa ni mtego uwenda dada amina kaingia ndani aone tena kuwa bado au naendelea na mchezo mchafu.
"Erinest nakueshimu sana naomba kaa mbali nami unataka nini tena kwangu au unataka kunikorofisha tena na dada amina kwa mara nyingine tena au?" 
Erinest alibaki akinitizama kwa maneno niliokuwa nimekwisha kuongea mda huo basi 
nae alibaki akiwa kwenye mshangao mkubwa lakini mimi sikujali nae akasikika akisema 
"usifanye hivyo isabela wajua fika kila kitu"
"Erinest yaliopita sindwereeeeee tugange ya jayoooo hayo ya nyuma achana nayo angalia ya sasa" Nilimjibu Erinest huku nikipatia mafumbo makali mnoooo 
"wa maanisha nini hapo Isabela?" aliuliza Erinest 
"kwa sasa Erinest mimi na mtu mwingine na siku si nyingi nitamleta kwenu kumtambulisha" 
Nilipoongea tu hivyo shem Erinest alibaki akiwa ana shangaaa na ndipo nilipo geuka kuanza kupiga hatua za kutoka ndani ya nyumba Erinest alinishika mkono na kusema
"usemayo ni kweli au?
"ndiyo tena ni ukweli toka moyoni kwa sasa niko na mpenzi" nilimjibu Erinest
Basi nami nilitoka nje ya nyumba hiyo na kugeuka tena kuitizama mara mbili kutokana na kile kilicho tokea ndani ya nyumba hicho kilinifanya kuwa na furahaaa huku nikimuombea dada amina kuwa na ukarimu kama huo tena na tena.
.
.
.
Nilirudi nyumbani kwa Erick na nilipofika niliingia ndani na kumkuta Erick akiwa sebureni basi ilinibidi nikae nae ili kumueleza kila kitu kilichokuwa kikinipa shida na msongo wa mazwazo lakini nae alikuwa muelewa na alinielewa.
Zilipita siku kazaaa na maisha yangu yakawa mazuri na yenye furaha kwani Erick alionekana kunijari na kunipatia kile nilichokuwa nataka na kwa wakati sitahili na ilibidi tufanye mipango ya kufunga ndoa huku kikwazo kikaonekana kuwa baraka za wazazi zinaitajika nami kuwaza kufunga safari na Erick mpaka kijijini kwetu nilipo zaliwa lakini yote nilimuhusisha dada yangu Yolanda kwa yote nilio kuwa naenda kufanya basi Tulisafiri mimi pamoja na Erick mpaka nyumbani na nilipofika tu nilikuta kijiji kimebadilika mpaka kupelekea kupotea nyumbani mpaka mwanakijiji mmoja alitusaidia mpaka kutufikisha kwetu huku Erick akiniona kuwa sikuwa na pakumbuka nyumbani kwetu.
Tulipofika majira ya mchana mama hatukumkuta na kumkuta kaka yangu Gabriel nae aliponiona tu  alifurahi sana 
Gabriel "dada Isabela karibu sana"
isabela "Asante Gabriel"
Gabriel "mda sana dada mpaka kupelekea kukusahau"
Isabela "yaaaah! kaka lakini sikupata nafasi ya kuja huku"
Gabriel "wasa dada wala usijali japo umerudi hakuna tatizo lolote"
Isabela "mama kaelekea wapi"
Gabriel "Yupo shambani toka asubui lakini mda hiii ndio huwa narudi"
Nilimkaribisha Erick kiti huku mizigo nikiipeleka ndani ili kumsubiria mama arudi toka shamba.
Nae mama alifika kutokea shamba basi nae alipofika karibu na kutuona alianza kuimba kimira huku akitukaribisha kwa shangweeee na alipofika moja kwa moja alikuja kwangu na kunishika huku aniniamgalia sana mwili wangu na kunizunguka.
Mama "mwanagu! mwanangu! mwanangu! isabela karibu sana"
isabela "asante mama"
Mama "mwanangu kipi kilikupelekea mpaka kusahau kwenu"
isabela "mama mambo madogo tu mama lakini nimekuletea mgeni mama umuonae mbele ya macho yao"
Ndipo mama alisalimiana na Erick na kunivuta pembeni na kuniuliza nami nilimwambia ndiye niliye mchagua basi mama alijawa na furaha sana kwani hakutegemea.
Basi niliingia jikoni na kuandaaa chakula ambacho tulijumuika wote mimi pamoja na Erick mama na kaka yangu Gabriel. 
Zilipita siku mbili tukiwa nyumbani mimi pamoja na Erick tuliaga huku mama aliweka baraka zake juuu ya ndoa yetu na kurudi mjini.
Erick alifanyaa mpango wa kufunga ndoa nayo mipango ilikuwa ikienda vizuri mpaka hapo siku ilipo wadia nami kwenye shera pembeni yangu Erick akiwa na suti nzuri kupita kiasi chake basi tulifunga ndoa na kuitwa mama huku nikibahatika kupata watoto wawili John pamoja na Heriet.
.
.
.
"Na ndipo ndoto yangu ya kuitwa mama ilitimia siku hiyo!!!!!!!!!!!!!!! nami kujifunza kuto waacha wtoto wangu kutanga tanga na maisha huku nikiwawekea msingi wa kuwa na HEKIMA"   

............................................ MWISHO................................................
.
.
COMING SOON "UTAMU WA TUNDA"

Share on Google Plus

About storynzuri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

7 comments:

  1. i enjoyed the story...thanks Hans
    coz ulinifanya niwe busy kukufatlia so itakuja nyingine au ndio bac tena

    ReplyDelete
  2. Huuuuuuuuuuuu!!!! Story nzur sana! Ur great unakipaj keep it up! Nasubir "Utamu wa Tundaaaaaaa"

    ReplyDelete
  3. One among story Kali nlizosoma hii ni moja wapo..

    ReplyDelete