Logo Design by FlamingText.com
Logo Design by FlamingText.com

storynzuri sehemu ya hamsini na tisa shemeji ingiza pole pole


..
. sehemu ya hamsini na tisa
.
Mtunzi INSTAGRAM @hanscharlz @storynzuri

ilipoishia ""Leo usiondoke mwambie dada yako hupo huku sawa nataka tuzungumze vizuri usiku"
"mmmmmmmh sawa Erick" nilimjibu huku nikiwa najuwa kuwa sina mahari pa kulala hiyo itakuwa ndio nafasi yangu.
.
.
Basi alipo kwisha kusema hivyo naye aliondoka na kuelekea chumbani kwake na kuniachia mimi jukumu la kumwambia tena dada lakini laiti angelijua kuwa sina mahusiano mazuri na dada Amina angeli furahia siku zote kuwa nami!. nami nilitoka jikoni na kuelekea chumbani kwangu huku nikingojea usiku huo kuwa ana nini anataka kuniambia lakini wakati nikitoka jikoni kuelekea chumbani nilikutana na Alex 
"samahani Isabela kwa kuchelewa kuja mezani kwani nilikuwa na uchovu mwingi"
"ohhooo! usijali Alex wala mimi sina neno lakini mimi na Erick tumekwisha maliza  lakini chako kiko pembeni hapo mezani"
"okay Asante Isabela basi nami naelekea huko huko"
"okay sawa ngoja nami nikapumzike"
Tuliachana huku mimi nikielekea chumbani nae kwenda mezani kupata kile nilichokuwa nimekiandaaa pamoja na Erick. Nilifika chumbani na kujitupa kitandani na kubaki nikihesabu masaaa tu yapite kwa siku hiyooo. 
Nilishituka mchana mishare ya saa nane na kutoka chumbani huku nikiwa na wazo la kwenda kubeba masalia yalio bakia kwenye hoteli nilipofika sebureni sikumwona mtu yoyote na kupata wazo la kutoroka ili nikifika tu na kurudi basi nami nilifanya hivyo na kwenda mpka hotelini na nilipofika Reception waliniuliza jina na nikawatajia huku wakidai kuwa chumba hicho wamesha mpa mtu mwingine.
"samahani dada mimi nilikuwa na ishi kwenye chumba namba 129 kwa kipindi cha nyuma kidogo lakini hapa kati nilikuwa nyumbani lakini wakati naondoka sikuchukuwa vitu vyangu vyotee kwani mda nliokuwa nimelipa hulikuwa bado haujafika tamati hivyo leo nimekuja kuvichukua" 
Umesema waitwa Isabela naona taharifa zako hapa kuwa uli sahini wakati wa kutoka na kwa sasa kuna mtu kachukua chumba hicho" aliongea muhudumu huyooo
"okay sawa lakini vipi kuhusu vitu vyangu naweza kuvipata?" 
"vitu vyako havipo kwani kuna mtu alikuja juzi kukuulizia na kuvichukua vitu hichooo"
"ni nani huyoo!" nilimuuliza swali huku nikiwa na jibu la kuwa ni shem Erinest tuuuu basi nilisubilia apekuwe na kutaja jina hilooo
"Erinest" alijibu muhudumu 
.
.
Nilibaki nikiwa na shangaaaa sana huku nikimfikiria shem bado yuko ananitafuta "nifanyeje mimi" nilibaki nikijiuliza mara nyingi sana swali hilooo huku nikikosa majibu na kuwaza kumwambia tu Erick endapo akija kujua asije kuniona muongo mimi. 
nilimuaga muhudumu huyo na kuondoka kurudi kwa Erick na nilipofika nyumbani tu Erick alikuja mukukumkuku mapaka nilipo na kuniuliza 
"Isabela ulikuwa wapi mwenzio nimejawa na mawazo sana"
"samahani Erick kwani niliona nikiwaaga nitawasumbua kwani nilikuwa najua nitarudi tu ondoa hofu kwa hilo sawaa"
"okay sawa isabela"
Niliingia tena chumbani mwangu huku nikiwaza ya kuwa nitamwambia vipi ukweli Erick nae kunielewaaa, Niliumiza kichwa sana huku nikiona endapo nikimwambia Erick Ataumia sana lakini niliona hakuna namna nyingine ya kumwambia ilinibidi nisubilie mda aliokuwa kaniomba nitakapo onana nae nitamwambia yote.
Usiku ulifika na tulipo maliza kula chakula sote tulielekea vyumbani mwetu huku tukiwa tumehakikisha kuwa nyumba yote imefungwa basi nilipokuwa chumbani nilimsubilia Erick mpaka ilipofika majira ya saa 5 usiku nae aligonga mlango.
"hallloooo ni mimi Erick Isabela"
"nakuja"
Nilifungua mlango nae kuingia ndani na alipoingia ndani nami kuufunga mlango na kurudi kitandani 
"Isabela sio kamba nimekuja kwa kuuvuruga usiku wako lakini imenibidi nije maana asubui ulinionesha vitu nami kuvutiwa navyoooo"
"mmmmmmh Erick vitu vipi tena mimi nilikuonesha jana" nilijifanya kuwa nimesahau huku nikitaka nione alivyo shupavu kwenye kutoa madini mdomoni
"Isabela inamaana kwamba ujajua kile kilichotokea kati yangu wakati tukiwa tuna andaa chakula"
"niambie tu Erick uwenda nimesahau" 
"okay sawa ni kuhusu hisia zangu ulizifanya kuwa kwenye msukumo ambao sikujua kabisa nifanye nini wakati huo"
.
.
Ilinibidi nijiongeze kuwa anataka nini wakati huo na ndipo nilipo mwambia
"Erick nikuulize kitu?"
"ndio niulize Isabela"
"Unanipenda kweli"
"yaah isabela nakupenda kupita kiasi kwani fikira zangu zote zakuwaza wewe kila kukicha?"
"nashukuru kusikia hivyooo lakini ningependa kukufahamisha ukweli juuu yangu kuwa kwa sasa mimi nilikuwa sikai kwa dada Amina"
"mmmmh kivipi yani na ulikuwa ukikaa wapi? aliuliza kwa mshangao sana Erick 
"nilikuwa nimepanga na ni storia ndefu sana Erick kwani kulitokea kuto kuelewana kati yangu na dada Amina ndio nikachukua jukumu la kutoka na kwenda mahari kupanga na mpaka sasa niko hapa"
"okay sawa basi tutakuwa wote pamoja sawa"
"lakini naomba kama unanipenda usije nifanyia visa mbeleni nikaja kuumia bure na ni bora kuniambia mapema"
"sitofanya hivyo Isabela kwa maana mimi na mpango wa kuoa na chaguo langu nimelipata ambaye ni wewe isabela naomba uniamini sita fanya hivyo uzaniavyo wewe"
Nae alipo maliza kusema hivyo nae alisogea na kunikumbata huku nikiwa naonekana kuwa dhaifu kwake kwani wanawake tuliumbwa hivyo.
Basi nilimuomba tutakaa chini na kuongelea maswala yote yatakayo tuhusu mimi na yeye.
nili lala na kulipokucha kama kawaida tuliendelea na maisha huku mahusiano yetu na Erick yalianza.
.
.
Zilipita siku kazaa huku tukiwa tunaishi vizuri mimi pamoja na Erick huku mahusiano yetu yalianza kushamili kwa kasi kubwa huku nikisahau yale ya shemeji Erinest na ndipo siku moja ilinibidi nitoke na kwenda kwa dada amina huku nikiwa nawaza pindi tutakapo kutanisha sura zetu lakini sikujali kwa hilo kwani nilikuwa naenda kwa ajiri kwenda kupatana na dada kwani nilijiona na makosa japo kuomba samahani kwa yale yaliyotokea.
Nakumbuka siku hiyo ilikuwa ni siku ya wikendi majira ya mchana na kufika kwa dada Amina na kuugonga mlango wake nae Erinest kuufungua mlango na aliponitizama tu allishangaa sana
"mmmmh Isabela karibu"
"asante"
"ingia ndani lakini Amina katoka kidogo"
"okay sawa wala usijali shem"
Niliingia mpaka sebureni na kukaa kwenye kochi nililikuwa nimelizoea na sikukaa saa nae dada Amina aliingia ndani na alipofika na kuniona 
"umefata nini hapa naomba utoke kwangu isabela"
Nilishindwa kuongea kwani dada amina alizidi kurusha maneno ambayo yalipelekea mpaka mimi kuanza kulia na ndipo nilipo piga magoti huku nikimfata dada amina na nilipo mfikia nilimshika miguuu nae alinisukuma na kudondoka chini lakini sikutaka kukata tamaa na kurudi tena huku shem Erinest akiwa yuko pembeni akitizama kile kilichokuwa kikiendelea.
Nani nilizidi kumwomba msamahaa dada amina lakini nae alianza kulia tu huku akiishiwa nguvu huku akikosa maneno kwani nae aliangua kilio huku nami pia nikiangua kilio hicho.
Na ndipo dada amina alinyanyuka na kuniangalia sana huku mimi nikiona aibu sana kwa kile nilichofanya nami niliona chochote atakacho hamua kwangu sawa nae alinyayua mdomo wake na kuanza kuniambia?

JE NI NINI AMINA ALITAKA KUMWAMBIA ISABELA?

WHATSAPP +255 652486818


.
......................STARBOY....................
Share on Google Plus

About storynzuri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

6 comments: