GANDA LA NDIZI
SEHEMU YA KWANZA
MTUNZI @hanscharlz @storynzuri
Whtsap +255652486818 Tsh 5000#
.
Ilikuwa siku ya Jumatatu kama ilivyokuwa ikizoeleka
kwa binti RECHO kudamka asubui na mapema na kwenda sokoni basi siku hiyo
alichelewa kufika sokoni na kukuta baadhi ya wachuuzi wenzake kuwakuta
wakiendelea na kupata vile walivyokuwa wakiviitaji na kwenda kuviuza kwenye
masoko yao madogo madogo, binti RECHO alipofika maeneo yale alishangaa sana
kuona vitu alivyokuwa akitarajia kuchukua kwa siku hiyo vilikuwa vikienda
kuisha basi nae alifanya upesi na kupata kile alichokuwa kafata japokuwa
kilikuwa ni kidogo sana lakini hakuwa na budi ilimbidi achukue tu. Alichukua na
kuweka kwenye ungo wake na kuzunguka zunguka japo kuona kama anaweza pata
mahari pengine kuongezea kile alichokuwa kapata kwa siku hiyo, binti RECHO
alizunguka sana mpaka hapo alipohakikisha kuwa kalizika na kile alichokuwa
kabeba basi nae alianza safari yake taratibu huku akiimba nyimbo zilizokuwa
zikimfanya aweze kufanya kazi kwa bidii na juhudi kali. Alipiga hatua kazaa na
kukutana na mteja wake wa kwanza siku zote na ndipo aliposhusha bidhaa zake na
kumtolea achague huku akisisitiza “vya le oleo hivyo mteja wangu” sauti ile
ilisikika kwa mteja yule nae kuanza kuchagua kile alichokuwa akipenda.
“kweli hizi ndizi ni za le oleo wala si uongo RECHO”
“hahahahaha ndio mteja wangu” alicheka Binti RECHO
huku akifurahia kile alichokuwa akifanya mteja wake akichagua huku akimsifia
“leo nachukua hivi tu”
“sawa ngoja nikufungie” alijibu Binti RECHO
Alipomaliza kumfungia binti RECHO alishika kifaa chake
na kuendelea na safari lakini kabla ajamaliza kuvuka eneo la mteja yule alisikia
sauti ikimpa sifa zake…
“na kesho upite niwe wa kwanza maana hizi ndizi ni
tamu kweli….”
Nae binti RECHO kusikia vile aligeuka nyuma na
kumtizama kisha kwendelea na safari yake lakini alimshangaza sana mteja wake
pale alipkuwa akitembea kwa malingo huku akirusha makalio yake basi mteja yule
alibaki akitizama na kushindwa kula kile alichokuwa akiendelea nacho mpaka hapo
alipofika mbali binti RECHO……
Aliendelea kuimba nyimbo zake huku akifikilia kuwa
siku hiyo atauza sana kwani mzigo wake ulikuwa ni mdogo sana huku pia akiwaza
pale wengine wakikosa huduma kwa siku hiyooo…….!
0 comments:
Post a Comment