.
SEHEMU
YA TANO
MTUNZI HANS CHARLZ
instagram @hanscharlz @storynzuri
Whatsapp +255652486818(10000 Tsh)
.
.
Na kulipo kucha jogoo wa shamba aliwika huku binti
NAMALA alikuwa mtu wa kwanza kufumbia macho yake kwani alikuwa ameshazoea
lakini kwa upande wa Bwana TUMBAKU hata sauti ya jogoo yule hakuweza kuisikia
kitu hicho kilimpelekea binti NAMALA………
.
Binti NAMALA aligeuka na kuwa mtu wa ajabu na kubaki
akimshangaza bwana tumbaku pale alipo shituka na kutaamaki kwa kile alichokione
mbele yake huku akijiuliza ni mkosi gani uliomuangukia….
“NAMALAAAAAAAAAAAAAAAAA!” aliita jina lile huku
akibaki amepigwa na butwa! Kumwona binti NAMALA akitililika jasho kali na huku
nguvu za kibinadamu zilikuwa zikipotea. Alianza kutetemeka bwana TUMBAKU huku
maneno yakimwisha na kubaki mdomo wazi huku akitafuta njia ya kuchomoka mahari
pale kwani alishituswa na kile alichokiona.
“hahahahahahahhaha” ni sauti iliokuwa ikisikika
pembezoni mwake huku naye bwana TUMBAKU akiifatisha sauti ile ghafura alipokuwa
akitupa macho yake pande zote alishangaa kujiona kuwa yuko mahara pasipo fahaa
kuwa yeye kwani aliona makaburi yakimzunguka na huku akizidi kumtizama binti
NAMALA alivyo kuwa akibadilika na kuonekana na kubaki mfupa tu kwenye mwili
wake.
Binti NAMALA naye alianza kutoa sauti za ajabu huku
akiwa kifuani mwa bwana TUMBAKU na kumweka roho juu kwani ilifikia mahari Bwana
TUMBAKU alipoteza kumbukumbu na kubaki akiwa amefumba macho yake lakini
hazikupita dakika alishituka…..! na………… .
.
Na kutazama tena kwenye kifuaa chake na kuona mifupa
tu ikiwa imemuegama nae ilimbidi achukue jukumu la kujitoa ufahamu kwani haikuwa
kazi nyepesi aliumia ujasili nae kuweza kuisogeza mifupa ile na kiwili wili cha
binti NAMALA…….
“Ni mkosi gani huu jamani umenikuta” ni maneno
yaliokuwa yakimtoka kimya kmya moyono mwake huku akiwa na lengo moja tu la
kutokomea mahara pa kupata msaada..
“HAAAHAHAAHAHA!!!!!!!!!!!!” ni mara ya pili sauti ile
ikisikika ikicheka kwa kishindo kikali na kumfanya bwana TUMBAKU kutotaka
kujivuta vuta mahara pale na kuweza kuitupa ile mifupa iliokuwa imemuegama
kifuani mwake…
“nini hiki tena” alijikuta akitoa sauti bila ya
kutojijua kuwa sauti yake ilikuwa ikisikika maeneo yale.
Aliwaza na kufikiia sana ni nini afanye kwa wakati ule
huku akiwa ka kwisha ondoa masalia mifupa ya NAMALA iliokuwa kwenye kifua
chake, ndipo wazo likamjia akimbilie upande wa kasikazini mwa mkono wake.
Alianza kupiga hatua kuelekea alipokuwa akiwaza ni
mahara salama lakini ilisikika sauti nyingine ikizungumza….
“Njia unayokwenda si sahihi chukua njia nyingine” nayo
sauti ilikata gafra na kumchanganya bwana TUMBAKU huku akiachilia mbali aliona
ni vyema kuifata njia ile licha ya kuwa na uoga mwingi ilimbidi afanye vile
kwani hakuwa na uelewa wa mahari pale.
Alichomoka kwa spidi kali huku ikimfanya ageuge nyuma
kuangalia usalama na ndipo alipo……..?
.
Alipogeuka na kutazama kivuli kikimfata kwa spidi kali
ae alipozidi kuchanganya kasi ilimbidi ajifiche pembezoni mwa barabara ilia one
mwisho wa kivuli kile lakini kilipokuwa kikizidi kumfata nacho kilizidi kufifia
kiasi cha kwamba mpaka alipomsogelea maeneo yale alipokuwa kajificha kilikuwa
kimekwisha potea chote. Bwana TUMBAKU alishangaa sana kuona maajabu yale huku
wazo lake tu ni kufika nyumbani kwake…..
Aliwaza sana yale yaliomtokea wakati akitizama huku na
kule ni wapi apite ili aweze kutokomea ili aweze kufika nyumbani… ilimchukua
mda kidogo huku akifikilia ni njia ipi aweze kupita wakati ule gafra alishituka
pale alipo sikia kitu kikimgusa maeneo ya nyuma huku kikimfanya kujua ni kile
kivuli kilichokuwa kikkimfata nae ndipo alipo geuka huku akiwa amejaa uoga…..!
alishangaa sana kuona nguo yake ikiwa imenasa na kusababisha kuhisi kuwa ni
kitu kilikuwa kikimpapasa maeneo ya mgongo wake.
Alijawa na hakili ya haraka pale alipopata njia na
kuanza safari yake aliochukua mda mchache na kufika kwenye kijiji chake. Wanakijiji
na ndugu zake walishangaa sana kumwona Bwana TUMBAKU akiwa kwenye hali ile
ambayo kila mmoja alitafsiri kivyake licha ya ukweli alikuwa akiujua bwana
TUMBAKU mwenyewe, nae hakuongea wakati ule na kupitiliza moja kwa moja mpaka
mahari anapolala nae kulala moja kwa moja na alipoamka ndipo alipo waita ndugu
zake ili kuwa simulia mkasa wote uliomkuta……………..!
“ndiyo hivyo ndugu zangu nisingeweza kurudi leo hii”
alizungumza na kujutia kile alichokifanya kwa binti NAMALA na kuwasisitiza
vijana wenzake kutoiga kile alichokifanya kuwa ni hatari kwa maisha yao
Basi kila mmoja wao pale alielewa na kubaki wakiyaweka
akilini yale aliokuwa akiwaambia bwana TUMBAKU na wote kutawanyika kurudi
kuendelea na shughuri zao huku somo wakiwa wamelielewa kile kilichomkuta ndugu
yao……………
MWISHO
0 comments:
Post a Comment