GANDA LA NDIZI
SEHEMU YA PILI
MTUNZI @hanscharlz @storynzuri
Whtsap +255652486818 Tsh 5000#
.
Hakuwa na budi binti RECHO alizidi kusonga mbele ili apate
kifuta jasho kwa siku hiyo basi barabara nzima alikuwa akitamba kwa mwendo wake
mpaka kupelekea vijana wengi kubaki mate yakiwadondoka kwani binti RECHO
alikuwa akiwapelekea hamsha hamsha ambayo haikuwa ya kawaida kwa vijana hao. Vijana
walianza kumfata huku wakimpigia mayowe ambayo kwa binti RECHO kupata moto na
kuzidisha Zaidi na Zaidi….
Alizidi kuzunguka nyumba kwa numba na ndipo alipopita
mahara flani alisikia sauti ya kike ikimwita naye kugeuka na kuitazama sauti ile
ilipokuwa ikitokea mara gafla alimwona mama mmoja akimfata huku akiwa ameshika
pesa mkononi. Binti RECHO alisimama na kumsikilaza mama yule kumbe naye alikuwa
akihitaji huduma nae kushusha chini chombo chake……..
“vyote vyaa leo leo mama” ni sauti ya binti RECHO
ikisemezana na mama yule..
“hoooo hata mimi naona mwanangu tena zimekomaa ni bei
gani hizi leo..”
“mama hapo utanipa kwa kila moja kiasi cha pesa mia
mbili tu (200#)”
“mwanangu ni nzuri lakini naomba unipunguzie”
“sawa mama unachukua ngapi?”
“leo nachukua kumi tu mwanangu”
Mama alichukua ndizi pamoja na matunda mengine
aliokuwa nayo binti RECHO na kurudi nyumbani kwake kwani alipokuwa akiishi hapakuwa
mbali na pale…., RECHO alikusanya vitu vyake na kuweka kwenye mpangilio mzuri
na kubeba chombo chake na kuendelea na safari yake ambayo aliona mapema kuwa
huwenda atamaliza.
Alizidi kuwa shawishi wateja wake siku hiyo huku
akionekana kuwa mchanga mfu sana kwa wateja wake hali hiyo iliwapelekea wateja
wake kwa siku hiyo wawe wapole tu huku ikionekana huwenda siku hiyo alipata
bahati yote hayo yalikuwa ni mawazo ya wateja wake…
Alipita mahali alisikia sauti na kugeuka nyuma
kuitazama na alipoiona tu…………….?
ITAENDELEA KESHO MDA KAMA HUUU!
0 comments:
Post a Comment