.
.
UTAMU WA TUNDA SEHEMU YA 23
MTUNZI HANSCHARLZ
INSTAGRAM @hanscharlz @storynzuri
Whtsapp +255 652486818 kwa 5000# tu.
.
Ilipishia
“hahahahhahaha sawa”
alicheka na kumminya sehemu ambayo kijana Hans alipata raha huku akimwambia
“hapo hapo Happy”
.
“mmmmmmh wapi Hans?
“juu kidogo ya
kiuno………!” Hans alijibu huku akivuta ule
utamu uliokuwa ukipenyeza kwenye mgongo wake
Happy aliendelea kumpa
kitu roho inapendaaaa mpaka hapo alipoona kijana karithika na kumwacha atulie
kidogo, Hans aliona kuwa mbimba ya binti Happy ilikuwa ikizidi kushika kasi
pale alipokuwa akiipapasaa na kuijulia hali.
“Happy naona mimba
inashika kasi vipi wazazi wako wanajua”
“hakuna hata mmoja
anayejua Zaidi yangu na wewe”
“kwanini sasa Happy
wafanya hivyo huku unaona kuna vitu vinataka kukwamisha ndoto zetu?”
“no Hans mpenzi wangu
wewe usijali”
“mambo makubwa haya
Happy”
“yah! Najua”
Hans alibaki akimwangalia
Happy kwa kile alichokuwa akifanya kwa siri mdogo mdogo Hans alipata usingizi
na kusahau kuwa alikuwa anatakiwa kwenda kwenye mizunguko huku Happy akizidi
kuchezea mwili wa kijana Hans, Happy alikuwa kwenye kipindi kigumu huku akili
yake ikiwaza sana siku ilikuwa umepangwa kufunga Harusi na kijana Clinton
kufanya uamuzi ambao alikuwa akiujua mwenyewe kumsaliti kijana Hans au
kumuumiza kijana Clinton. Naye yalipopita masaa kazaa huku akiwa getoni mwa
kijana Hans huku akiona kuwa mda ukizidi kuyoyoma ilimbidi achomoke kurudi
nyumbani, alimwacha kijana Hans huku akikoroma kitandani mwake naye kurudishia
mlango na kuelekea nyumbani Happy alifika nyumbani na kuingia ndani lakini
aliokuwa akikatiza kolido la sebureni naye alisikia sauti ya mama yake
ikimwita.
“Happy Happy
Happy………………….!”
“abe mama”
“mbona siku hizi mbili
tatu unatoka bila y ahata kuaga”
“Hapana mama nilikuwa
hapo kwa rafiki yangu tu”
“rafikiiiiii?”
“ndiyo
mama”
“sawa” naye Happy alijibu
na kuelekea chumbani mwake
.
.
Baba Happy alirudi kutoka
kwenye mizunguko yake naye alikuja na jipya pale alipomwita mama Happy pamoja
na binti yao Happy nae kukaa nao wote ili wazungumze juuu ya kile kilichokuwa
kikiendelea juu ya binti yao pamoja na kijana Clinton.
“nimewaita hapa juu ya
swala lla kijana Clinton nab inti yetu Happy”
Baba alizungumuza maada
ile Happy alishituka na kungoja kile kilchokuwa kikiendelea baba aliendelea
tena kuongea, “tuko pamoja mpaka hapo”
“ndiyo mume wangu” mama
aliitikia huku Happy akiwa mdomo umejaa mate hawezi kutoa sauti yake,
“jumamosi hii kwa mujibu
wa upande wa pili Harusi itafungwa hiyo nikutokana na kijana Clinton kuwa
likizo yake ya kukaa hapa bongo itakuwa inafikia tamati hivyo siku hiyo ndiyo
imeteuliwa kuwa ya kuwaaga vijana wetu kwenye maisha yao mapya”
“Baba Happy mbona mapema
mno”
“weeeeeeee? Mapema…” Baba
aliuliza kwa jaziba huku akimtolea mama Happy macho makali, ukweli Baba Happy
alitokea kubadilika sana sio kama kipendi cha nyuma mama Happy alikuwa akiwaza
hayo.
“ndio mume wangu”
“basi ndiyo tumepanga
kutokana na kijana wao kutaka kuondoka nab inti yetu”
“sawa Happy tuko pamoja”
Happy alishindwa kujibu
na kunyanyuka kwenda chumbani mwake na alipofika alilia sana huku akiwaza “nini
baba anafanya kwangu” ni maneno aliokuwa akiyatoa kinywani mwake huku
akichuluzisha machozi yaliokuwa yakienda moja kwa moja mpaka sakafuni, Baba
Happy alibakia na mkewe sebureni huku akiendelea kutasimini juu ya siku ya
Harusi ya mtoto wao, ndipo Baba alipo mpa jukumu mkewe kwenda kumfanya mtoto
wao ili asije kuwaaibisha siku ya Harusi kwani walimjua fika binti yao
alivyokuwa kichaaa asiki wala kuelewa.
Mama alikwenda moja kwa
moja mpaka chumbani mwa Happy na kuanza kumtuliza
“mwanangu kubali tu
kuolewa na kijana Clinton hana neno mtoto wa watu”
“mama we acha tu ujui
ndio maana”
“sawa lakini Baba yako
anakutengenezea mazingira usije teseka mbeleni”
“sawa mama” Happy
aliitikia vile kumlizisha mama yake naye mama kutoka chumbani mwake.
.
.
Zilipita siku kazaa huku
ilikuwa imebakia siku moja kwenda kufanyika Harusi ya Clinton na Happy mtaa
mzima ulijua kuwa binti Happy Harusi yake ni siku iliokuwa ikifuata, basi
vijiweni usiku Hans katika pita pita yake alikutana na maada hiyo iliokuwa
ikizungumziwa Harusi inayo kwenda kufanyika ni ya kimataifa kwani vijana
waliokuwa wakizizungumza walikuwa wakitia na chumvi kiasi chake
“heeeee mtoto mmoja hapo
kati mzuri kishenzi kesho Harusi yake”
“heeeeee yupi huyo
mwanangu” kijana mmoja alidakia
“si yule aliokuwa
akiutikisa sana mtaaa wa hapo nyuma”
“mmmmmmmh nani huyooo…?”
“haaaaaaah kumbe yule
binti Happy” aliitikia kijana wa pembeni
“yah mwananngu ndio huyo
huyo”
Hans aliposikia vile
aliendelea kusikiliza na kuwaza kwani siku mbili hizi hakuweza kuonana naye
binti Happy na kuwaza kuwa binti Happy kaonesha udhaifu mkubwa, naye aliingilia kati mjadara ule kujua ni lini
na wapi Harusi itafungwa.
“hivi harusi ya huyo dada
inafugwa wapi” aliuliza kijana Hans
“kanisa la ushuwani…”
alijibu kijana aliyekuwa akijua na mahari gani panapo fanyika harusi ile
Hans alitoka mdogo mdogo
mpaka getoni mwake na kujitupa kitandani mwake na kuitafuta picha aliowai
kumpatia kipindi cha nyumba binti Happy naye alianza kuitazama huku akifikilia
zile za chinichini alizokuwa akimpeleka binti Happy kwenye kilele, aliwaza sana
ni wapi atapata kuponea kama sio kwa binti Happy alipitiwa na usingizi mpaka
asubui.
Kulikucha siku ya
Jumamosi nayo familia ya Baba Happy ilianza maandalizi ya mwanao kwenda
kanisani huku mda ulikuwa umepengwa kwa wawili hao kufunga ndoa ulikuwa
ukishika kasi pale ilipofika saa sita mchana, kwa upande wa kijana Hans naye
alichelewa sana kuamka kwani alikuwa kalewa chapaka chapa naye alipoona masaa
yakizidi kushika kasi alichomoka kitandani na kuanza kuzikamata njia za
kwelekea kanisani………..
Ilipofika wakati Clinton ndani
ya suti pia Happy ndani ya shela huku wakisindikizwa na zigeregere na vifijo
mpaka mazabauni mbele ya padre Clinton alimvua shela binti Happy ili wamalizie
hatua ya mwisho, padre alianza kubaliki ndoa ile huku ikifata sauti za wawili
hao kukubaliana kuwa mwili mmoja katika maisha yao…..
“Clinton pamoja na Happy
sogereaneni” ni maneno yaliokuwa yakitoka kwa padre
“ndugu Clinton umekubali
kumpokea binti Happy awe mke wako wa kufa na kuzikana….”
“ndiyo nakubali” aliitikia
kijana Clinton
“nawe Happy unakubali
kuwa na Clinton awe mume wako wa kufa na kuzikana”
Ukimya ulitawala kwa
binti Happy huku padre akingoja tamko la binti Happy naye alirudia kwa mara ya
pili gafra sauti ilisikika ikitokea nyumaaaaaaa…….?
.
JE NI SAUTI YA NANI
ILISIKIKA?
0 comments:
Post a Comment