.
.
UTAMU WA TUNDA SEHEMU YA 24
MTUNZI HANSCHARLZ
INSTAGRAM @hanscharlz @storynzuri
Whtsapp +255 652486818 kwa 5000# tu.
.
Ilipishia
“nawe Happy unakubali
kuwa na Clinton awe mume wako wa kufa na kuzikana”
Ukimya ulitawala kwa
binti Happy huku padre akingoja tamko la binti Happy naye alirudia kwa mara ya
pili gafra sauti ilisikika ikitokea nyumaaaaaaa…….?
.
“Happy unanisalitiiii” ni
sauti ya kijana Hans ilikuwa ikisikika huku akisogea eneo la tukio,
Waumini na wote waliokuwa
kwenye misa hiyo walipigwa na butwaa pale binti Happy aliposhindwa kuvumilia na
kutoongea nae kutoka mbio mbele kwenye madhabau na kumfata kijana Hans, Nae
alipomfikia kijana Hans aliwageukia waumini na wageni waalikwa nae bila y ahata
woga alizungumza…..!
“huyu ndiye nilie
pendezwa naye” aliongea maneno yale machache bint Happy na kumshika mkono
kijana Hans kutimuka wote kutoka ndani ya kanisaa.
Wazazi wa pande zote
mbili walibaki wakiwa kwenye mshangaoo wa hali ya juuu huku mama Happy alikuwa
akilaanai sana huku akimlalamikia mumeweee kwa kile alichokuwa akitaka
kifanyike sasa kinawatia aibu…
“mume wangu nilikuambia
mtoto yule alivyoooo…!”
“mke wangu sikujua haya
yote”
“sasa unaona hizi sura
zetu tunazificha wapi?”
“mke wangu mda huuu si wa
kulalamiiana” Baba Happy aliongea maneno yale huku akiinamisha kichwa chake kwa
ile aibu iliokuwa ikimsonga kichani mwake, basi nae ilimbidi apite mlango wa
nyuma ili kukimbia umati ule.
Kijana Clinton alibaki
akishangaaa huku akiwa na padre wakiwa madhabauni wawili hao walikuwa
wakishangaana naye padre ndipo alipo muuliza kijana Clinton
“kulikoni mke wako au
mlikuja kuongopa mbele ya kanisa”
“hapana padri mpaka sasa
sijui kipi kinachoendelea”
“ujui…?”
“ndiyo sijui lolote
mwenyezi mungu ananiona”
Watu waliokuwa kwenye
misa hiyo kila mmoja alitawanyika na kuiacha familia ya Clinton huku
wakitafakali kile kilichotokea huku na kule walimtazama Baba yake Happy wala
hawakuweza kumwona kwani alikuwa ameshakwisha pita mlango wa nyuma na
kuondoka..!
“aibu hiii mke wangu
tunaificha wapi” Baba Clinton alizungumza
“kweli hiii aibu mno watu
tumewapotezea mda wao wanatuona si sio wa maana”
“mpaka rafiki yangu
kakimbia” aliongea huku akishika kichwa naye kuchukua simu yake iliokuwa mfukoni
na kumpigia Baba Happy, simu ilipokelewa naye hakuanza na salamu bali alimwagia
madingo baba yake Happy mbele ya umati aliokuwa nao huku nao walikuwa
wakimpandisha hasila naye kuikata simu huku akiendelea kulalamika kwa kile
kilicho tokea, Basi nao walikuwa wamepoteza hela nyingi kwaajili ya kijana wao
kuoa basi iliwabidi warudi nyumbani.
.
.
Happy pamoja na Hans
walizidi kutimua mbio huku wakielekea mahara pa utulivu na walipofika mahali
hapo walipumzika napo kulikiwa na upepo mzuri tena miti iliokuwa ikidondosha
maua mazuri ambayo yaliwafanya kukaaa hapo mpaka makija ya jioni huku wakipiga
story za kile kilichotokea kwa binti kutaka kumsaliti kijan Hans .
“Happy kwanini ulitaka
kunisaliti” aliuliza kijana Hans
“no Hans wala sikuwa na
nia hiyoo”
“inamaana nisinge kuja
pale ndio ungekuwa mke halali wa yule kibalaka”
“no Hans sijui tu lakini
sikutamani iwe hivyo kwani name nilipokuona tu nilijawa na nguvu za kuweza
kuongea chochote”
“mmmmmmh sawa”
Mama Happy pamoja na
mumewe walirudi nyumbani huku kila mmoja wao alipita njia yake…
Walianza kuojiana kuhusu
mtoto wao alipokimbilia basi kila mmoja wao hakuweza kujua mahali alipo naye
mama alikuwa akijua mahali alipokuwa akiishi kijana Hans naye mama alitoka na
kwenda kumtafuta binti yao lakini cha kushangaza hata alipofika hakuweza
kumkuta mtu kwani geto la kijana Hans lilikuwa limewekewa kufuri zito
lilimwacha mama Happy kuwa kwenye mawazo kweli basi alianza kurudi nyumbani
huku akiwa mnyonge lakini alipozidi kuiacha geto la kijana Hans alimwona Happy
pamoja na kijana Hans wakiwa wanarudi naye aliwasubilia mpaka wafike kwani
ndiyo ilikuwa njia ya kufika kwenye geto la kijana Hans.
“Mamaaaaa! Unafata nini
huku” Happy alimwona mama naye huku kijana Hans alitaka kukimbia naye Happy
alipo mshika mkono wake huku akimzuia, mama alimsogelea mwanae Happy…….
“Happy nini ulichofanya…?”
“Mama toka mwanzo mimi
niliwaambia kuwa sijapendezwa naye”
“hata kama mwanangu sio
kwa kile ulichokionesha leo”
“mama kila mtu huwa na
haki ya msingi kuuseea moyo name ndivyo nilivyo fanya”
“hata twende nyumbani”
“mimi mama siendi
nyumbani namuogopa Baba”
“kwa kipi hasa unamuogopa
baba yako”
“si kwa tukio zima la
leo”
“mweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!
Ebu twende nyumbani”
Mama aliongea huku
akimtizama kijana Hans alivyokuwa kavaaa nae Happy pamoja na mama yake
waliongozana kuelekea nyumbani, na walipofika walimkuta baba kichwa kikiwa
kimejaa asila naye alipo mwona tu Happy alianza kupayuka ovyoo mpaka mtaa wa
pili ulisikia kwa zile kelele zilizokuwa zikiendelea.
“Happy nini
umefanya………….”
“Baba moyo wangu
haukulizika na Clinton…..!”
“ohooooo! Kumbe ndiyo
kijana yule anakufundisha jinsi ya kujibu wazazi wako”
Hapana Baba lakini sikuwa
tayari kwa kile mlichokuwa mkifanya juu yangu name nilikuwa nikikataa lakini
hamkuweza kunisikiliza kwa kile nilichokuwa naitaji Dady”
Baba alichoka na kushusha
pumzi huku akilegeza Tai aliokuwa kavaa huku akiona kuwa ikimbana sana, ndipo
Mama Happy nae akaja juu huku akimlalamikia mme wake juu ya kile alichokuwa
akifanya juu ya mtoto wao Happy na ndipo Baba alipo choka na kumwamulu binti
yao Happy kumwita kijana Hans kwao ili aje kuwaona wazazi ili awe mume alali wa
binti yao
“Basi sawa namuitaji
kijana huyo kesho sawa………”
“kweli Baba…..”
“ndio” Happy aliposikia
vile moyo wake ulijawa na furaha kuwa Baba yake mzazi naye kalizika kuwa na
Hans basi furaha zake zote alizikimbiza chumbani mwake huku akiuchezea mto huku
akizidi kumkumbuka kijana Hans alivyokuwa akipeleka mashambulizi kwenye lango
lake, kulikucha asubui sana Happy alichomoka nyumbani kwao na kuelekea kwa
kijana Hans nae alipofika getoni mwa kijana Hans alipitiliza na kumkuta yuko na
taulo lake basin aye alikaa pembeni yake huku akifurahi kupita kiasi huku
akimtizama mara nyingi nyingi kijana Hans huku naye Hans alizidi kujiuliza ni
kipi hasa juu ya binti Happy nae alifumbua kinywa chake nakuongea………….
“Vipi Happy kulikoni
furaha zote hizi…”
“Ungekuwa moyono ungejua
nini na furahia Hans.”
“Mmmmmh nambiye basi na mimi”
Happy alizidi kutoa
tabasamu lililozidi kumchanganya kijana Hans na ndipo alipo mtazama huku
akishika nyuso yake na kuzungusha mikono yake huku akipa maneno mazuri…..
“baby Baba kakubari na
leo kaomba twende nyumbani mimi pamoja na wew”
“heeeeeh kwenu Happy?
“ndiyo baby” Happy
aliongea huku akimsisitiza kijana Hans kuwa wazazi wake walikuwa wakimuuitaji….
“naogopa mpenzi”
“wanipenda kweli” ni
maneno yaliokuwa yakimtoka binti Happy huku yakifatana…. Huku yakimuamasisha
kijana Hans kujibu huku akijiamini….
“ndiyo nakupenda tena sana
Happy”
“basi naomba fatana nami leo
mpaka nyumbani”
“okay sawa” Hans alijibu
kwa kishingo upande huku akijua kuwa happy alikuwa akimtania….
.
.
Hans ilimbidi ajiandae
vizuri naye Happy alikuwa na pesa kiasi alizokuwa kachomoa kwa wazazi wake basi waliingia mtaani kwenda kumtafutia
kijana Hans japo nguo nzuri naye aonekane kuwa nazifu pindi atakapo kutana na
wazazi wa binti Happy, walifanikiwa kupata mavazi yaliokuwa yakiendana na siku
ile basi nao walirudi kwenye geto la kijana Hans na kubadilisha nguo ili
waongozane na Happy mpaka kwao ili aonane na wazazi wa binti huyoooooo!. Walitoka
na kuanza kupiga hatua kuelekea kwao na Happy huku kijana Hans alikuwa ajiamini
kama ni kwelia au alikuwa akiota lakini binti Happy alionekana kuwa na nguvu
lape alipokuwa akiongea nae huku akimfanya kuwa na ujasiri wa kuongea na wazazi
wake licha yake kuwa muuoga…
“karinu Hans…………………”
Happy alimkaribisha kijana Hans mpaka ndani
“asante japo mwenyeji
hapa”
“naomba nisubilie hapa
dakika chache sawa mpenzi…”
“sawa” Hans alijibu huku
akiwa na huoga mwingi kwani alikuwa akimwogopa sana mama yake na Happy
Happy alitoka na kwenda
kuwaita wazazi wake waliokuwa chumbani, nao waliposikia kuwa kijana Hans
kawasili basi walitoka chumbani na kwenda moja kwa moja mpaka sebureni, na
walipofika walimkuta kijana Hans akiwa tofauti na walivyokuwa wamezoea basi
muonekano ule uliwafanya wazazi washituke na kumwona kuwa kijana mtanashati….
“karibu kijana”
“asante….” Aliitikia huku
akitizama chuni huku akiwa hajiamini
“kwanza hongera sana
kijana umeonekana kuwa na ndamu nzuri iliompendeza mtoto wetu basi nasi
tumelizia kuwa naye…….
“asante baba” Hans
alizidi kutojielewa mpaka wakati huo na ndipo alipoitwa Happy
Basi walipomaliza
kumkabizi kijana Hans nao walijumuika kwa pamoja kwa chakula kilichokuwa kimeandaliwa
nab inti mzoefu Johari, basi Hans alianza kuzoea huku wakicheka na wazazi wa
binti Happy. Katikati ya tafrija ile binti ndipo alipo zihilisha kuwa yuko na
mimba ya kijana Hans wazazi wake walishanga japokuwa mama yake alikuwa akijua
kila kilichokuwa kikiendelea basin ae Baba hakuwa na lolote la kufanya kwani
alijuwa wazi binti yao kaishakuwa nae alipopewa taharifa ile wala hakuweza
kuijia juu.
Ulipita mwaka mmoja huku binti
Happy pamoja na kijana Hans kupata mtoto mmoja wa kiume huku wazazi wake Happy walisaidia
sana huku waliwajengea nyumba nzuri na maisha ya kijana Hans yalibadilika pale
baba Happy akimwajili kwenye kampuni yake na kumpa kitendo kijana Hans, naye
Hans alizidi kuonesha juhudi kwenye kazi huku akimflaisha bosi wake mpaka alipo
pandishwa cheo na kuwa na kitengo kikubwa….., Maisha yake yalikuwa mazuri huku
akimfanya Happy ndiye jicho lake……………….. huku akilisamini mnooo
……………………………………….MWISHO…………………………………………………..
Nime ipenda story..uko vizuri
ReplyDeleteFootball Predictions Mpesa
..Keep up the good work !
Best story
ReplyDelete