Sehemu ya therasini na nne Mtunzi IG @hanscharlz.@storynzuri . Ilipoishia "ok sawa isabela nitategemea kupata call yako" . Nilishuka ndani ya gari hilo lilokuwa limesheheni harufu nzuri zenye kuchanganya na kuvutia mno. Huenda pengine yalinichanganya akili yangu kisawia kwani yalikuwa yakinukia na yalipenya mpaka ndani ya nafsi yangu na niliposhuka kwenye gari hilo basi nae aliondosha kwa speed ya hatari huku kila mtu alibaki akiitizama nami pia nilibaki mdomo wazi huku vumbi zito likionekana maeneo hayo basi ilibidi kumtizama mpaka alipoishia na ndipo nilipokumbuka card alionipa na kuitizama tena huku nikifikilia mengi juu ya hiyo lakini nilitupa moyo konde na kuingia ndani ya saloon na kuanza kufanya usafi. Basi nilipokuwa nikiendelea kufanya usafi wangu ndani ya saloon basi kitu kilinipitia na kuwaza huku sauti ikisikika masikioni mwangu ya yule kaka aliyekuwa kanipatia msahada wa lifti siku hiyooo kwenda kazini huku ikizidi kusisitiza nimtafute. Nilikaa chini na kuwaza mnooo huku nikiwa nimeishika card hiyooo na ndipo nilipo chukua simu yangu kwenye mkoba wangu huku nikijikuta nikiijaza ile namba ya yule kaka lakini mara gafra nilipotaka tu kupiga tu moyo ulisita na kuwaza kanipa mda huuu na kumtafuta mda huuu huku nikiwaza uwenda atanichukulia vibaya na ndipo nilipoikata na kuizima simu hiyo na kuirudisha ndani ya mkoba na kuambatanisha card nikiokuwa nimepewa pia niliitunza ndani ya mkoba wangu. Usafi nilimaliza kufanya na kusubiria wateja ili niwaudumie basi hata wateja sikuwazungumzia sana nao walianza kufika maeneo yangu ya saloon huku mmoja moja wakija nao gafra walionekana kuwa wengi nami kazi ilianza kuwaidumia na kuwapa huduma kwa siku hiyoooo. Wakati nikiendelea na kazi mara nyingine tena gafra nikamuona dada amina akija kwa speed kama siku iliyooopita na alipofika kama kawaida nae aliniomba tuongee faraga mara moja huku akisisitiza ni kitu cha muhimu sana nami niliwaomba hudhura wateja wangu na kumfata dada amina na kumsikiliza lakini siku hiyo alikuja tofauti na siku ile na ndipo alipoanza kuniuliza maswaliii. "Isabela mdogo wangu wewe ni kama ndugu yangu kwenye nyumba yangu chochote lazima nikushirikishe lakini kwa hili nalo kwenda kukuambia?"
0 comments:
Post a Comment