GANDA LA NDIZI
SEHEMU YA SITA
MTUNZI @hanscharlz @storynzuri
Whtsap +255652486818 Tsh 5000#
.
Alishangaa sana kuona binti mrembo akipiga yowe
liliambatana na mtikisiko mkali pale alipokuwa anajitaidi kujiokoa licha ya
kijana yule aliyekuwa na baisikeli nae kuiendesha kwa kasi ili kuweza kumsaidia
japo kumshika kwa nyuma ili asiweze kudondoka chini lakini jitihada za kijana
yule ziligonga mwamba pale alipomshika vibaya nae kuyumba yumba na baisikeli
yake.
“yesuuuuu na malia” ilisikika sauti kutoka ndani ya
jengo nae alikuwa ni kijana aliye tupa GANDA LA NDIZI chini pasipo ruhusiwa
Alitoka mbio kijakazi wake ndani aliposikia bosi wake
akilalama peke yake huku akichungulia… na alipofika alishanga kumwona bosi wake
macho yakiwa nje nae akiwa salama ndipo alipo mwambia bosi wake…
“kulikoni tena bosi wangu mayowe hayo wakati huu!”
“mmmmmh natajaza nje hapa kunatukio limetokea mda huu”
“tukio!!!” aliuliza kwa mshangao mkubwa sana
“ndio wewe njoo ujionee mwenyewe” alijibu na kuendelea
kutazama
Kijakazi nae mbio mbio na kufika alipokuwa kasimama
bosi wake na kutizama huku nae akibaki kushangaa.
“kimetokea nini bosi mbona sielewi” aliuliza tena
kijakazi
“GANDA LA NDIZI”
“GANDA LA NDIZI!!!!!!!!!!!!!!!!!”
“ndio GANDA LA NDIZI” bosi alijibu bila wasi wasi
wowote na kuendelea kutizama
“twende tukawasaidie basi”
“siwezi kwenda mimi ndio chanzo cha hilo tukio”
alijibu bosi na kuingia ofisi kwake
Basi kijakazi alishinda kwenda kwani alimwona muajiri
wake karudi ndani nae ilimbidi afanye hivyo kwani alikuwa akipenda kazi yake
huku akiohofia huwenda akienda eneo lile anaweza kupoteza ajira yake…..
Kijana yule pamoja na jitiada zile lakini mambo
yalienda mlama pale alipozidiwa na uzito wa mrembo yule na kukubali matokeo ya
kushinda kuhimili uzito ule….. Na ardhi yote ilisikia kwa kishindo kikali kilichotokea
na kuwaacha watu waliokuwa maeneo yale kuwa kwenye sitofahamu……..?
0 comments:
Post a Comment