Logo Design by FlamingText.com
Logo Design by FlamingText.com

GANDA LA NDIZI sehemu ya TANO

GANDA LA NDIZI
SEHEMU YA TANO
MTUNZI @hanscharlz @storynzuri
Whtsap +255652486818 Tsh 5000#
.
Basi VICK alizidi kuzisogelea ofisi zake nae hakuwa na ili wala lile alizidi kusogea mdogo mdogo lakini cha ajabu hakuweza kuona mbele yake kwani alikuwa akipiga macho yake chini tu huku akitembea. Nae binti VICK alichukua simu yake na kuiweka vizuri ndani ya pochi wakati alipokuwa akiweka kijana yule aliyekula ndizi za binti RECHO asila zake aliona ni heli kutupa GANDA LA NDIZI barabarani na kuondoka. VICK hakuwa na ili wala lile nae alikuwa spidi kali huku akisogea eneo lile alilokuwepo kijana yule licha ya kijana msamalia kuona tukio zima mbele akiwa kwenye baisikeli yake alipiga yowe huku akimtaka binti VICK apite upande mwingine…..
“dadaaaaaaa!!!!!!!!!” aliita kijana yule kwa sauti ya juu
Licha ya jitiada zote zile alizoonesha kijana yule binti VICK hakuweza kusikia huku nae akiwa na mawazo ya ndizi ile aliokula basi hakuweza kusikia chochote.
Kijana yule aliyetupa GANDA LA NDIZI aliondoka eneo lile na kurudi ndani ya ofisi yake huku akilalama sana juu ya kile kilichokuwa kimetokea mpaka kijakazi wake alipoona vile naye alimuuliza
“kulikoni bosi wangu” aliuliza na kumsogelea mahali alipo
“hakuna kitu chochote” naa alijibu huku akionesha kuwa hana tatizo wakati ni mwenye mawazo teleeee
“bosi unaonekana kuwa na mawazo sana nambie uwenda nikawa msaada wako” kijakazi alizidi kumuuliza bosi wake
“nimekuambia hakuna kitu endelea na shughuri zako ndani sawa”
“sawa bosi” alijibu na kuwa mpole na kurudi mahali alipokuwa na kuendelea na shughuri zake huku akimwacha bosi wake akishika tama
Hazikupita dakika nyingi wakati ule kijana yule alisikia sauti nje ikipiga yowe na kelele nyingi, alinyanyuka huku akiwa mvivu naye alijilazimisha na kusimama vizuri na kwenda nje na alipofika alishangaa sana kuona……..
USIKOSE SEHEMU INAYO FATA HAPA HAPA MDA KAMA HUU


Share on Google Plus

About storynzuri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment