GANDA LA NDIZI
SEHEMU YA TATU
MTUNZI @hanscharlz @storynzuri
Whtsap +255652486818 Tsh 5000#
.
Alimwonamtu akimwita kwa hishara ya mkono naye
hakuweza kupoteza mda alisogea eneo alilopo kijana huyo na alipofika tu
alishusha kifaa chake na kumsogezea ili achague kile alichokuwa akihitaji….
“karibu sana vyote vya le oleo hivyoooo kaka angu…!”
aliongea huku akionesha kujali wateja wake
“sawa dada yangu name naona ni vya leo leo”
“kunamatunda mbali mbali wewe unapendelea nini?” RECHO
alimuuliza kijana yule
“haaaaaah! Binti wewe unanionaje mimi nipatie kitu
kizuri kama ulivyoo wewe”
“mmmmmmh sawa leo ndizi ziko vizuri waweza kuchukua
kwani zinamvuto mzuri..” alijibu huku akiongezea chumvi nyingi kwenye biashara
yake…
Ndipo kijana alipo chukua pesa mfukoni na kuitoa ili
ampatie binti RECHO lakini aliacha madoido pale alipokuwa akichepeza pesa yake
na kuonesha kwa binti RECHO kuwa anapesa nyingi ili hali aweze kumshawishi
kwani alianza kumpa meneno madogo tena matamu huku nia yake ikiwa apate kwa
usiku mmoja. Lakini kwa binti RECHO hakuweza kufanikiwa pale alipoanza kumwona
wa kawaidi alipokuwa akijigamba…
“kijana wewe mimi sio wa mchezo mchezo……”
“hahahhaha kwanini binti mzuri…”
“unaona mimi wa kupenda pesa heeee” alibadilika binti
RECHO pale pale na kumwacha hoi kijana yuleeeeee!!!
“sio hivyo mrembo kwani umemanisha vibaya tu”
“sawa nipatie pesa yangu mimi niondoke” binti RECHO
aliomba kwa nguvu pesa yake na kijana yule alionekana kutamani makalio yake
huku akijisemea moyoni binti RECHO. Aliona ni bora kudai haki yake pale pale
bila ya kufanya mambo mengine….
Kijana yule kwa kumkomoa binti RECHO alitoa noti ya
pesa kubwa ili hali binti RECHO aone uvivu kwenda kuitafuta lakini haikuwa vile
alivyokuwa akizani kijana yule ndipo RECHO alipochukua pesa ile na kwenda duka
la pembeni alipokuwa na kuomba msaada ili asaidiwe kuvunjiwa pesa ile….
“samahani kaka naomba unisaidie kunivunjia pesa hii”
ni sauti ya binti RECHO ikimbembeleza kijana yule
“sawa ni ya bei gani hiyo pesa”
“elfu kumi tu (10000) za kitanzania”
“okay sawa lete nikusaidia dada yangu”
Alifanikiwa kupata msaada na haraka haraka kurudi
kumpatia pesa iliokuwa imebaki. Kijana yule alishangaa kumwona RECHO akiwa ni
mwingi wa furaha na kujua tu kafanikiwa basi sura yake ilibadilika na
kumwangalia sana RECHO lakini binti RECHO wala hakuwa na wasiwasi wakati ule…………….?
0 comments:
Post a Comment