GANDA LA NDIZI
SEHEMU YA NNE
MTUNZI @hanscharlz @storynzuri
Whtsap +255652486818 Tsh 5000#
.
Basi binti RECHO alishika chombo chake kwa umakini wa
hali ya juu na kuangalia pande zote huku akiona ziko shwali basi ilimbidi
achukue maamuzi magumu pale alipochomoka kwa sipidi ya ajabu mpaka kupelekea
kijana yule kubaki akipigwa butwaaa Zaidi ya dakika kazaa zilipita huku
akimtizama binti RECHO….. alishika kichwa chake na kugeuka ili aendelee na
shughuri zake mahali pale basi alimenya ndizi ya kwanza na kula pale pale
aliona ni tabu sana na kubaki akimtizama mpaka alipoisia binti RECHO..
RECHO alizidi kupiga hatua zake nyingi mpaka kupelekea
kujikwaaa lakini amanusura adondoke lakini kwa uwezo wake na mzoefu wa mazoezi
zoezi la kudondoka lilishindwa.
Alisonga mbele lakini wakati akitokomea mara gafra
alikutana na binti mmoja aliyekuwa akijulikana kwa jina la VICK. VICK nae
alikuwa akielekea kazini majila hayo ya asubui licha ya kupenda sana ndizi za
binti RECHO ilimbidi amsimamishe lakini alipokuwa akidiliki kumwita binti RECHO
alimwona kuwa mawazo yake hayakuwa mahali pale basi alimgoja na kusimama mbele
yake na kumshitua….
“kulikoni ndugu yangu mawazo yanatoka wapi?” aliongea
VICK na kumwacha binti RECHO akitizama nyuma nae kumwona kuwa huwenda
anakimbizwa basin ae aliona ni heri kutupa macho yake kule alipokuwa akiangalia
binti RECHO. Hakufanikiwa kuona kitu licha ya kumwona kijana mmoja akiendelea
na mambo yake basi alimshika mkono binti RECHO na kumwambia……………..
“kulikoniiiii leo biashara unauza kweli….”
“ndio dada yangu” alijibu huku akiwa na mashaka
mwilini mwake
“sawa mbona unaangalia sana ulikotoka kulikoni”
Hamna chochote!!!! Matunda ni ya leo leo dada yangu”
alikata maongezi yale na kuingia kufanya biashara wakati huo….
“hata mimi naona ni vya lee leo ni bei gani leo”
“kama kawaida dada bei haijabadilika ni ile ile”
alijibu RECHO
“naomba tunda moja nionje hapa” alipewa nae kula na
alipomaliza alilipa pesa na kuendelea na safari………………..
VICK alipiga hatua zake huku akila tunda lake mpaka
pale alipolimaliza na kushika kasi kuelekea kazini kwake….
0 comments:
Post a Comment