Logo Design by FlamingText.com
Logo Design by FlamingText.com

storynzuri sehemu ya hamsini na moja shemeji ingiza pole pole



.
.
.
Sehemu ya hamsini na moja
Mtunzi INSTAGRAM @hanscharlz @storynzuri
.
ilipoishia "kwa mujibu wa wasamalia walioona tukio hilooo na raia wema waliojitokeza kumleta mpaka hapa lakini walikuja wagonjwa wapatao watano (5) ambao miongoni mwao alikuwa ni Erick huku Erick ndiye alie pona kwenye ajari hiyooo huku wengine walifikishwa hapa wakiwa wameshapoteza uhai."
.
Daktari aliendelea kunisimulia yote yaliyo tokea kwenye ajari ya Erick huku nikiwa namsikiliza kwa umakini mnoo! na kuniacha nikiwa na wazaaa sana juu ya yale yaliokua yamempata Erick na rafiki zake wa nne nami nilimuomba mungu apate nafuu kwani kwa mujibu wa dokta ulikuwa ukionesha kuwa yeye ndiye aliyekuwa kapona kati ya hao watano. Ilinilazimu kuwa ndiye mtu wake wa karibu japo kuwa daktari nilimdanganya nae hakujua chochote juu yetu nae alifata kile nisemacho na kukiamini. Basi alipokwisha kunisimulia daktari nae alinishitua kwa kuniita kwani akili yangu ilikuwa mbali sana wakati alipokuwa akinisimulia huku akiniambia "Isabela tuko pamoja"
Nami ilinibidi niitikie tu kwa kuwa yote aliokuwa akinisimulia nilikuwa nimeyaingiza japo kuwa mengine siku yaweka "Tuko pamoja daktari nimekuelewa lakini naomba japo fanya chochote juuu ya mgonjwa wangu"
Ndipo daktari nae alijibu bila wasiwasi huku akinitia moyooo juuu ya kumuhudumia Erick "sawa Isabela wala usijali kwa hilo ndio kazi yangu nami nakuhakikishia kwa lolote litakalo tokea nitakujuza chakufanya nipatie namba yako ya simu kwa mawasiliano zaidi"
Nilimpatia namba yangu haraka haraka na nilipo maliza ilinibidi tena nirudi mahari alipokuwa kalazwaa Erick ili kumuona kwa mara ya mwisho ili nipate kuondoka na kurudi Hotelini ili nijipange vizuri kuja kumuuguza kwa kipindi chote hicho mpaka hapo atakapo pona basi nilifika na nilimkuta bado hawezi hata fungua macho yake uku akiwa kwenye mashine nilimwangalia huku huruma ikinijaaa mpaka kupelekea kudondosha chozi langu huku nikiwa nimeinamia kitanda chake na ndipo daktari aliponinyanyua na kunisihiii nirudi nyumbani kwani mda wa kuwaona wagonjwa ulikuwa umekwisha nami nilijikokota na kunyanyuka hapo huku nikipata msaada wa daktari na kumuacha Erick na kuelekea Hotelini kujipanga na siku itakayo fata.

Niliondoka na kumuacha daktari akiendelea kumuhudumia Erick huku daktari huyo akionesha kuwa ni mtu mwenye huruma sana kwani kwa sasa hakuna daktari angeweza kufanya alivyo kuwa yeye kiukweli nilimpenda kwa kile alichokuwa akionesha na kukifanya basi nami nilifika Hotelini mahari napo ishi huku nikiwa mwingi wa mawazo kwani sikutegemea sana siku kama hiyo ingekuwa na changamoto kiasi hicho zilizo onekana kuwa ni ngumu na tena ni zenye kufanya akili ikiwa inachemka basi sikuweza fanya chochote nilipofika tu ndani mkoba niliokuwa nimeubeba niliutupa kulia nami kuelekea kushoto kukitafuta kitanda huku na viatu pia navyo vilionekana kuwa vizito miguuni mwangu na kujikuta nikiwa mwepesi na kutokumbuka hata mahari nilipo vivua viatu hivyoo! na kujitupa kitandani na nilizidi kuangaika na kutapa tapa huku akili yangu ikiwa kwa Erick tu maana zile pesa zilinitia tumbo joto huku nikihisi nitakapo kuwa nae zitaondokana na matatizo ya dunia.

Nileendelea kuwaza juu ya yale yote yaliompata huku nikifikria kuwa endapo nikimpoteza nami mipango yangu itakuwa imefeli juuu ya yale niliokuwa nimekusudia kufanya pindi niwapo na Erick. Nilijikuta napitiwa na usingizi ambao sikujua umechangiwa na mawazo au lahaa! yote hayo sikujua pindi nilipo shitushwa na ndoto ilionesha kuwa inatafsiri mbaya huku nami sikujua ndoto hiyo ilichokuwa ikimanisha kwani upeo wa kufikiria na kuzitatua ndoto sikuwa nazo lakini muonekano wa ndoto nilioota ulinifanya kuwa inamaana mbaya basi ilinibidi niichukulie kama ndoto nyingine basi siku ilipita nami kulipokucha tu nilitoka asubui sana na kwenda sokoni kuangalia matunda japo nitakapo kwenda hospital niwe na kitu mkononi kumpelekea mgonjwa Erick. Nami nilifanya hivyo na kupata matunda mazuri na kufunga safari moja kwa moja mpaka hospital na nilipofika nilikuwa nimeshazoea chumba na mahari alipo lazwa Erick nami nilienda moja kwa moja kwenye kitanda alichokuwa kalala akipumulia mashine huku nikimtazama na hali yaki nilona haikuwa nzuri huku akiwa bado kupata kufumbua macho hiyo hali hata mimi iliogopesha sana huku nikipoteza asilimia nyingi za kuwa nae tena. 

Lakini nilipokuwa nikimtizama mara gafra niliingiwa na wazo nami ilinibidi nilifanyie kazi wakati alijapotea akilini mwangu huku nikisogea taratibu mpaka mahari alipokuwa kalala  Erick na ndipo kuona mkono wake mmoja ukiwa una cheza cheza nami nilipata nguvu za kuwahi na kuhakikisha kama ni macho yangu au kweli na kweli nipo sogea mkono wake ulizidi kucheza cheza na kunifanya kutoa tabasamu zuri huku nguvu zikinijia na kuushika mkono wake hapo hapo nilishituka kuona na macho akifumbua taratibu hapo hapo ilinibidi nikimbie moja kwa moja mpaka kwenye ofisi ya daktari na kumueleza juu ya kile nilichokuwa nimekiona kutoka kwa Erick akionesha hatua ya kwanza kufumbua macho takiribani siku 2 hakuweza. Nae aliposikia habari hizo tulitoka wote mbio kuwahi mahari alipo Erick lakini cha kushangaza nae daktari alipofika na kuona vile alitoa tabasamu huku mimi aliniacha kwenye njia panda na ndipo ilipo bidi kumuuliza 
"kulikoni daktali mbona unatabasamu huku ukifurahi kuna nini hapo maana umeniacha njia pandaaa"
Nae alinijibu "Isabela kwa kazi niliifanya kwa Erick mpaka kufikia hapa inanirazimu kuwa na furaha huku nikitoa yangu kwani nimepata tabu sana juuu ya mgonjwa huyuuu na kuna hatua inayo fuata ambayo kwangu na kwako itatutia hamasa ya kufurahi endapo tukifanikiwa? kwani hiii hali ni tofauti sana na ile aliokuja nayo"

Nami kusikia hivyo nilikuwa na shauku ya kutaka kujua na ndipo nilipo muuliza tena daktari 
"kwahiyo mgonjwa wangu hivi karibuni atakuwa vizuri na kuruhusiwa kurudi nyumbani au?"
ndipo daktari alipojibu juu ya swali langu "Ndio Isabela kwani alionekana kuwa na tatizo kubwa pale alipo pata ajari na kwa vile kaonesha hatua ya mwisho ambayo nimeiona mimi ni siku chache tu atakuwa yuko vizuri na kuruhusiwa kurudi nyumbani lakini mpaka hapo nitakapo chukua vipimo na kumuandikia dawa atakazokuwa akitumia nyumbani lakini kwa sasa ngoja nimwangalie kwanza kwa hili jambo ambalo umeniitia nione kama atachukua siku ngapi sawa Isabela"
Basi nilipo sikia hivyo nami moyoni nilikuwa mwingi wa furaha na mwenye shahuku ya kuruhusiwa huku pili nikiwaza atakapo toka je nitampeleka kwake au hotelini lakini laaaaha! sitofanya hivyo kwani itanilazimu kupajua kwake tu? nilijiuliza na kujijibu mwenyewe 
.
JE ERICK ATATOKA HOSPTALI NA KURUDI KWAKE AU HOTELINI KWA ISABELA? 
.
USIKOSE SEHEMU YA HAMSINI NA MBILI 
.
STORY WRITER INSTAGRAM @storynzuri 
.
.
...................................S T A R  B O Y..............................









  

Share on Google Plus

About storynzuri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

6 comments: