Sehemu ya kumi na saba
Mtunzi IG @hanscharlz @storynzuri .
Ilipoishia "nifungulie mlango kwanza nitakuelezea "
.
Nilifungua mlangu huo lakini sikutaka kumruhusu kuingia mpaka ndani na nikamuomba tuongere hapo hapo mlangoni.
Kumbe alivyokuja speed yote ile alikuwa kaota ndoto mbaya na kuona kitu kikimkimbiza ndotoni huku kingine kikimshitua ndotoni na ndipo alipokuja kuomba msaada huku nami alivyokuwa akinisimulia uoga ulinitawala mnoo.
Ilinipasa nimtulize kwani tukio hilo lililompata ndio mara ya kwanza kutokea kwenye nyumba hiyo. Nikihisi ni ndoto tu alioota ndio iliiomfanya aogope nami ilinibidi nimtulize na alipotulia kwa hofu aliokuwa nayo ilinibidi nimshike mkona huku tukiongozana mpaka kwenye mlango wake na nilipomfikisha anakolala nilimuacha nami kurudi chumbani mwangu kulala tena.
Nakulipokucha nami niliona siyo busara kutopita na kumjulia hali shem wangu nami nilijongea mpaka kwenye mlango wake ili.nipate kujua kalala vipi!
"hodi shem "
"Karibu isabela "
"asante vipi za toka jana kuhusu ndoto ile ilikupata tena shem "
"Nashukuru sana kwa kunitia moyo jana haikuendelea shemu wangu niko vizuri "
Nilimuaga pale alipokuwa kalala na kuanza kupiga hatua kadhaa ila nilipofikasha hatua chache sauti ya shem Erinest ikiniita nirudi mara moja tena.
Nilirudi kumsikiliza alichoniitia na nilipofika haraka haraka bila hata ya kungojea hata nifike tuongee shem Erinest alishuka kitandani kwa speed kali na kusogea karibu yangu na kunishika mkono hofu ilinitanda ha huku hisia zangu zikinijia kwa speed kali pindi aliponishika mkono ule na ikanibidi nivunje ukimya na kumwambia.
"Shem kulikoni au bado waogopa ndoto "
"Hapana shem lakini nikitaka tu nikushike mkono ila shem weweeeeeee!"
"Nambie Erinest vipi tena "
Alicheka kwa kicheko kikali sana nakuniambia tena.
"Shem bwana unamkono mzuri tena laini wenye kujua mapishi lakini daaah!"
"lakini nini tena shem "
"Mkono wako isabela "
"Umefanyeje tena shem mbona uko sawa "
Shem Erinest alionekana kunielewa na kunipenda lakini alikuwa akizunguka sana lakini aliponishika mkono ulee mashallaah! Mwili haukuwa wangu tena maana hisia zangu aliziteka na ziliamka na kuwaza vingi mnooo!.
Baada ya kuona hayo yakinizidi nilichomoka.
.
.
WAWEZA NI CHEKI WHTSAP +255652486818
0 comments:
Post a Comment