Logo Design by FlamingText.com
Logo Design by FlamingText.com

StoryNzuri Sehemu ya ishirini na tano Shemeji ingiza pole pole

.

.

Sehemu ya ishirini na tano 
Mtunzi IG @hanscharlz @storynzuri .
Ilipoishia "akusema wakati mda wa kuwasili "
.
Siku hiyo nilichelewa mno kuamka basi nilirudi ndani na kuingia jikoni kuandaa chakula huku hofu yangu ipo kwa dada amina atakapo kuja na kukuta hali iliyopo kati yangu na shem Erinest ilinibidi nijipe matumaini ya kutofahamu wala kujua chochote kati yetu mimi pamoja na Erinest basi niliendelea kufanya kazi jikoni huku nikiwa na mawazo hayoo. Nilimaliza kuanda chakula na cha dada amina ilinipasa kukitenga pembeni na pindi tu atakapofika akikute kikiwa na umoto wa hali ya kawaida na chetu nilipeleka mezani na kila mtu alipakua na kula hapo huku tukiendelea kupiga story za mwisho mwisho kati yetu.
Mlango uligongwa huku sote tukishituka na kujua tu ni dada amina kawasili basi nilinyanguka na.kuelekea mlangoni kuufungua na nilipofungua mlango huo nilikutana na dada amina huku akiwa kabadilika kiasi chake na kufikilia alipokuwa mazingira yalimpenda. 
Nilimkalibisha ndani nae aliingia na alipofika sebureni alimkuta shem Erinest na ndipo alipo mkimbilia huku nyuso yake ikiwa na furaha kwa kiasi chake kweli nilivyo muona dada amina alimpenda sana Erinest nakuwaza atakapojua itakuwaje nilitupa macho yangu tena mahari walipo na kuona wakikumbatiana kwa pamoja na ndipo shem Erinest alimsogezea kiti na Amina nae aliketi pia pembeni ya Erinest basi mimi nilibaki kushanga na ndipo nilipo kwenda jikoni tena kuchukua chakula nilichokuwa nimemwandalia na kumuhifadhia kwa umakini sana kwani alikuwa hapendelei vitu vilivyo vya baridi kwake sijui ilikuwaje. Nilifanya haraka nikatenga pia mezani ili tuendelee kujumuika nae kwani alitukutia katikati na hatukuwa tumemaliza kula. Nilipofika tu shem Erinest aliomba kijiko ili yeye ndiye atakaye mpakulia chakula hicho na kudai kumuhudumia yeye mwenyewe huku mimi kusikia hayo ilinibidi nikubaliane nae kwani alikuwa akionesha mahaba ya kumkaribisha mkewe Amina. Alimpakulia chakula kiasi akiweka kwa mbwebwe na madoido pindi alipokuwa akimlisha chakula.
Nami kuona hayo ilinipasa niondoke pale ili nikaendeleee na shughuri jikoni kwani siku hiyo ilinibidi nisitishe tu kwenda kazini (saloon ) nilitoka sebureni na kuwaacha wakiendelea.

Share on Google Plus

About storynzuri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment