Logo Design by FlamingText.com
Logo Design by FlamingText.com

storynzuri sehemu ya kumi na mbili Shemeji Ingiza Pole Pole Mtunzi IG @hanscharlz @storynzuri

Sehemu ya kumi na mbili 
Mtunzi IG @hanscharlz @storynzuri .
ilipooishia "Amina " "sawa nimekuelewaa ok "
.
alipokwisha kusema hivyo simu ilikatika gafra huku nikijuwa na mengine ya kuongea nae nilijaribu kupiga tena lakini simu haikuwa hewani tena niliingiwa na hofu huku nikitambua ya kuwa akikamatwa tu nami sitakuwa na mwelekeo wowote kweli siku hiyo sikuwa na amani sana huku mawazo mengi nikiwaza yale yaliotokea nafsi nao ikanambia nifunge saloon mapema na nielekee nyumbani ninakoishi na dada amina basi ikanibidi nifunge saloon na nielekee nyumbani. Nilipofika karibu gafra nilisimama huku nikishitushwa na wingi wa polisi wakishuka ndani ya gari na kuzunguka nyumba ya dada amina nami sikuweka woga wowote kwani nilikuwa nisha choka na naitaji nipumzike ilinibidi nisogee taratibu na nilipofika getini walinizuia kuingia ndani huku wakinioji maswali mengi huku dakika za mwisho walinikatalia kuingia ndani na kufunga mlango huku wakidai nyumba hiyo hawaruhusiwi kuingia mtu yoyote kuingia huku wakidai nyumba iko kwenye upelelezi. 
Walifunga mlango na kuniacha nalia sielewi pakuelekea kwa usiku huo nikiwaza kwenda kulala hotelini huku nikiwa sina pesa yoyote ya kunitosheleza mimi kwa usiku huo na ilinibidi nirudi tu saloon. Nilifika nakufungua mlango na kuingia ndani siku hiyo nililala saloon na kulipokucha niliamka kama kawaida na kuanza usafi lakini maji ya kusafishia alikuwa yameisha nami ilinibidi nichukue jukumu la kwenda kuchota maji mtaa wa pili. Nilitoka na ndooo ndogo na kuanza safari ya kuelekea kuchota maji nilipo pita mtaa wa kwanza nilishangazwa na kutaharuki kuona picha ya dada amina kila kona hiku ikioneshwa kuwa "WWANTED "
nilianza kuzungusha macho yangu pande zote na kuona picha hiyo imetapakaaa kila mahari na ikanibidi niwe yuda kwa mda mfupi kwani watu waliokuwa wakinijua wengi wao walikuwa wakiniangalia mno huku suea zao zikiwa na hasira sana nikiogopa mnoo pindi walipokuwa wakinifata na kuniuliza maswali mengi juuu ya dada amina nami niliikana picha hiyo mara tatu nilirudi saloon haraka haraka nikiwa sina maji wala nini! na kubaki nikiwa na mawazo juu ya swala hilo kwani nilihisi nami wanaweza kuingizwa kwenye kesi hiyo..?

Share on Google Plus

About storynzuri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment