MTUNZI : HANS CHARLES
Instagram @hanscharlz @storynzuri
SEHEMU
YA KWANZA
KULIPO
KUCHA KATIKA KIJIJI CHA KISHONKIZO
Ilikuwa Jumapili asubui
kumekucha kijiji cha KISHONKIZO jua lilichomoza kwa mbali huku likiashilia ni
siku nzuri basi, wanakijiji wa kijiji hicho wali damka asubui na mapema,
waliendelea na shuhuru za hapa na pale licha ya kijana aliye zoeleka kwa
uchapakazi mzuri kijiji hapo nae alijulikana kama KAPILO, ni kijana mchapakazi
sana na alipendwa na kijiji kizima kwa juhudi zake za uchapakazi na kukijenga
kijiji hicho, Nae siku hiyo alikuwa akitoka nyumbani kabeba ndoo ya maji kwenda
kwenye mto kuchota maji, ambayo alipanga kufanya shuguri zake siku hiyooo.
Alifika kisimani na
kuwakuta wadada wapatao watatu huku wakipiga stori juuu ya siku hiyo ilionekana
kuwa na sherehe, japokuwa kijana KAPILO hakujua kilichokuwa kikizungumziwa
mahali hapo na wadada hao nae alifanya yake na kuchota maji na alipo maliza kuchota
maji nafsi yake ilisita nae alitaka kujua kile kilichokuwa kikiendelea siku
hiyo japo yeye alikuwa nyuma kidogo kwani hakujua chochote, ndipo alipo
wasalimiwa wadada wale.
“Habari zenu wadada
wazuri muuuuh wazima wa afya”
“Wazima hofu kwako kijana
mchapakazi” walijibu wote kwa pamoja huku wakionekana kumjua vizuri KAPILO
“Samahani sana, wakati
nachota maji niwasikia mkizungumzia siku ya leo mwaweza nijuza name kuelewa”
kijana aliomba kujuzwa na wadada wale huku mmoja akinyanyua mdomo wake na
kusema “mmmmmh wewe kijana hujui kuwa leo kuna KIGODORO mtaaa wa MAPUNGE”
aliongea na kubaki akimtizama kijana KAPILO huku akimvutia kwa jicho zuri nae
bibti huyo alimkonyeza kijana KAPILO, huku nae kijana hakuweza kuendelea huku
akibaki mdomo wazi
“Asanteni na shukuru sana
kunijuza kwani name sikuwa najua chochote kile”
Nae kijana KAPILO akipo
kwisha kuwaaga alichukua ndooo yake na kuanza safari ya kurudi nyumbani lakini
cha kushangaza kila alipokuwa akipita aliona kijiji kiko bize na kila mmoja wao
akiendelea na shughuri zake, na alipo zidi kukatisha alianza kuona yale
aliyokuwa akiambiwa na madada wale aliokutana nae kisimani, alipozidi kusogea
alizidi kusikia mdundo wa ngoma ambayo ilikuwa ikipigwa kwa staili yake huku
ikiwa na ustadi wa hali ya juu, nae kwa mbali aliona vijana wakikimia sehemu
farani huku nae akielekea huko huko.
.
.
Alivyokuwa akizidi
kusogea mara alimwona kijana mdogo nae kumsimamisha ili amuulize kilichokuwa
mbele huku akiona vikundi vya watu vikizidi kumiminika mahari paliko kuwa
panasikika ndoma nzuri,
“Mbona wakimbia hivyo
kuna nini huko” alimuuliza kijana huyo
“Kuna ngoma” kijana huyo
aliongea hivyo na kutimuka huku aliona kuwa anacheleshwa na KAPILO
Ndipo nae KAPILO alipo
ona nae ni bora kuelekea asije kupitwa kwa kile akiskiacho, alizidi kupiga
hatua ndefu ili hali nae afike mapema kwani ngoma zile zilivyokuwa akizidi
kupiga hatua zake zilizidi mdundo huku sauti ya ngoma ile ilizidi kumchanganya
akili kwani hakuwai kusikia au kucheza alikuwa akisikia tu na kusimuliwa.
Basi alichanganya miguuu
yake haraka kuwai eneo la tukio lile na alipo karibia huku akiacha hatua chache
tu aliona kikundi cha mabinti warembo wakitia hamsha hamsha eneo lote lile,
huku nae akizidi kusogea na kuipita njia ya kurudi kwao, nae kijana KAPILO
alifika huku akibaki akishangaaa watu wakizidi kumiminika mahali pale nae
alijichanganya pasipo kujua anaelekea wapi,
.
.
Kikundi kile kilichokuwa
kimesheeni mabinti na vijana waliokuwa wakiuufanya mdundo usikike vizuri
walianza kuama mahali pale huku wakielekea mahala husika, nao wote waliongozana
huku wakimfanya kijana KAPILO kuungana nao kwani nae alivutiwa nao kwani
walikuwa wakibilinga bilinga makalio yao huku wakimwacha hoi bintabani kijana
KAPILO nae akawa “karatasi kifata upepo”, basi waliongozana kwa msafara huku
wakiimba nyimbo za vijiweni mchanganyiko huku wakitia madoido kwenye sauti na
mipazo ya sauti waliokuwa wakitooooa!!!!!!.
KAPILO alikwa kabeba
ndooo yake huku nae akiufata msafara ule unako elekea, huku walipokuwa walipita
walizidi kuwasomba vijana na watoto waliokuwa wakipenda “VIGODORO” kwani
kikundi hicho kilikuwa kikifahamika mno hapo kijijini kwa siku ya jumapili
kufanya tamasha mahali popote pale licha ya wazeee kuzuia walishindwa mpaka
wakaona njia nyingine ni kuwaomba mizimu ya kijiji hicho kazi nao wazee wa
kijiji hicho walipo sikia kuwa siku hiyo kuna “KIGODORO” walitisha kikao cha
dharula,
NINI KITAENDELEA USIKOSE SEHEMU INAYO FATA?
0 comments:
Post a Comment