Logo Design by FlamingText.com
Logo Design by FlamingText.com

storynzuriSehemu ya Tisa Mtunzi IG @hanscharlz @storynzuri

Sehemu ya Tisa 
Mtunzi IG @hanscharlz @storynzuri
.
Nilikubari japokuwa sikupenda iwe hivyo kwani nilikuwa nimemzoea sana Dada Yolanda lakini sikutaka kuwa na kipingamizi kwani walikuwa wakielewana ilinibidi niwape heshima yao na kuwakubalia yote waliokuwa wameafiki juu yangu kwani walipofikia tamati ya Mimi kwenda kwa boss Amina.
Sikuwa na budi ilibidi nifate wasemayo niliwaaga pale walipokuwa wameketi sebureni na kwenda chumbani kwangu kujipanga na safari ya kuhamia kwa rafiki yake Yolanda (Amina). Nao niliwaacha sebureni huku nyuso zao kila mtu zikiwa na tabasamu huku tabasamu LA boss Amina lilikuwa limefika lengo lake. 
Nilifikiria sana pale nilipo kuwa nikipanga Nguo zangu kwa ajili ya kuhama nyumba hiyo ya dada Yolanda na kuamia kwa Amina yote Yale nilikuwa nikiwaza sikupata majibu sahihi na kuwaza kuona yote heri kwani nilikuja mjini kutafuta maisha na ilibidi nifanye Yale wasemayo.
Kulikucha siku iliyo fuata nami nilijiandaa kwenda kwenye shuguri za kila siku yani saloon nilipo kuwa nikifanya Kazi huku nikiwa nimebeba Nguo zangu mbili tatu ili nikitoka jioni niunganishe kwa boss Amina.
Nilipo fika saloon majira ya SAA 2 asubuhi nilianza na usafi
Ndani ya saloon kama nilivyo kuwa nimezoea siku zote na nilipo maliza usafi ule nilipumzika kidogo na siku tumia dakika nyingi sana kupumzika alitokea mteja na aliomba nimuudumie nami sikuwa na budi ilibidi nichukue vifaa na kuanza kumuhudumia mteja huku tukipiga stori katikati ya stori zile alimuulizia Dada Amina.
Mteja "mpaka mda huuu boss wako haijafika tuu!!?
Isabela" ndio kwani aliniambia kuwa atachelewa kufika kutokana na majukumu mengine ya ki biashara.
Mteja "biashara sana au zile zile tulizo zizoea kola siku Ku achana na saloon....?
Isabela" sijui ila kwa upande wangu kaniambia hivyo!!!?
Mteja "kuwa makini sana Mdogo wangu na boss wako?
Isabela" kivipi Mbona waniweka njia panda Dada yangu nieleweshe...?
Mteja "usiwe na shaka kawaida tu utakuja kujua badae kwanza wewe Fanya shuguri zako zilizokuleta hapa saloon"
Alikwisha kusema hivyo mteja huyo huku Mimi nikiwa nimebaki na alama ya kuuliza(???) .

Share on Google Plus

About storynzuri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment