Logo Design by FlamingText.com
Logo Design by FlamingText.com

storynzuriSehemu ya Tano Mtunzi IG @hanscharlz @storynzuri .

Sehemu ya Tano
Mtunzi IG @hanscharlz @storynzuri
.
Ilipoishia "kama mama alivyo sema nilifanya upesi na nikiwa tayari kwa safari"
.
.
Tulianza safari mnamo majira ya jioni kuelekea mjini alipokuwa akiishi Yolanda safari ilichukua masaa mengi kiasi licha ya tulifika salama kwake lakini ilikuwa usiku sana basi kila mmoja alionekana kuwa mchovu sana. Mimi nilipofika tu si kupenda kuficha ile ofu ya ugeni kwani nilimuomba Dada Yolanda anielekeze bafu lilipokuwa ili nipunguze uchovu niliokuwa nao kwa wakati ule.
Aliniongoza mpaka bafuni na nilipo fika nilishangaa sana kuona maji yakitoka juu kumwagika kama mvua daaaaah! Nilibaki jicho kodoooo hofu na woga ulitawala pale Yolanda aliponiambia "OGA sasa uondoe uchovu nami nitaoga ukitoka wewe"
Maneno yale yalinifanya kuzidi kuogopa na ndipo nilipo jitoa ufahamu na kufungulia bomba. Maji yali churuzika kwa staili yake huku nikiwa nayazoea taratibu sikutaka kuwa na papala nilioga na maji ambayo yalinifanya nichukue mda mrefu kwani Yale maji yalikuwa ya moto kiasi chake na nilinogewa mnoooo! Nilimaliza kuoga.
Nilipo maliza kuoga Dada Yolanda alinipeleka kwenye chumba ambacho alikuwa kaniandalia kwaajili ya kulala na nilipo fika karibu na mlango alinikaribisha.
Yolanda "hapa ndipo utakapo kuwa unalala sawa mdogo wangu 
Isabela " sawa Dada"
Nikiitika kwa hofu sana kwani mahari nikipokuwa nimeandaliwa ili ni lale nilishangaa sana kuona vitu kama vile machoni mwangu.
Usiku kwangu ulikuwa mkubwa sana kwani kitanda nilichokuwa nimelalia kilinifanya ni sahau kilicho nileta kuwa ni elimu na kuwaza mambo ya dunia. 
Nilichelewa siku hiyo kuamka kwani nikizoea sana nyumbani kuamka mapema sana lakini kwa usingizi niliopata kutoka kwenye kitanda kile ulikuwa Wa aina yake. .

Share on Google Plus

About storynzuri

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment