storynzuriSehemu ya SitA
Mtunzi IG @hanscharlz @storynzuri
.
Ilipoishia "usingizi niliupata daah! Ulikuwa Wa aina yake"
.
Nilimkuta Dada Yolanda kaisha amka na nilimkuta jikoni akiandaa chai nami nilifika na kumsaidia Kazi zilizo kuwepo chache na tulipo maliza sote tulipeleka vyakula mezani kwaajili ya kifungua kinywa kwa siku hiyo ya kwanza kwangu na chakula nilicho kula siku hiyo duuh! Kilikuwa kitamu sana mpishi alinikaribisha vizuri sana.
Siku zilipita na maisha ya pale niliyazoea na kujikuta na fahamu mitaa mingi bila ya mwenyeji wangu Yolanda kwani Yolanda hakuwa mtu Wa kutoka na kutembea mitaa ya pale.
Dada Yolanda alianza mipango ya kunitafutia shule ili nami nianze masomo haraka iwezekanavyo. Siku hazikupita nyingi Dada Yolanda alipata shule na kunisii nifanye maandalizi ya siku 2 nianze masomo. Ilifika majira ya mchana siku hiyo hiyo alionipatia shule na kuniomba nitoke nae kidogo tuka zurule. Alinipakiza kwenye gari lake na kuanza safari ambayo sikujui niendako nami sikuwa na hofu nae basi nilikuwa mtulivu mpaka alipo simamisha gari na kunambia.
Yolanda "tumefika Mdogo wagu"
Isabela "sawa dada"
Sikuelewa mahali pale na kubaki nashangaa kuona vitu ambavyo sijawai kuona. Tuliingia kwenye Duka moja LA Nguo mjini (sahara) na tulivo ingia nae aliniambia chochote nikionacho na macho yakakipenda ni sisite kumwambia kwani dhumuni LA kunileta hapo dukani ni kunifanyia shopping.
Turizunguka na nilichokuwa nikikiona nami siku sita kuchukua kama alivyokuwa kanambia nikionacho kizuri nijiudumie mwenyewe. Alinifanyia shopping moja kubwa sana kwani mtoko nilipata mingi sana huku nikikumbuka kilicho nileta ni elimu na siyo mambo mengine basi Dada Yolanda alilipia kile nilicho chukua dukani mule na kuanza safari ya kurudi nyumbani tulipofika nyumbani nilihisi kama miujiza imeniangukia Mimi na mwaka huuu nitakuwa mtu tofauti ("yote hayo nikijisemea moyoni").
Nilianza shule huku siku ya kwanza nakumbuka nilikuwa muoga kwani uoga ulichangiwa na ugeni wangu shuleni hapo lakini kadri siku zilivyo kuwa zikisonga mbele nilizoeana na wanafunzi wenzangu na kuonekana kuwa kipenzi cha wote kwenye masomo yangu. Nilipo fika kidato cha pili nilifanya mtiani Wa kuingia kidato cha tatu.....
About storynzuri
0 comments:
Post a Comment