storynzuriSehemu ya NNE
Mtunzi IG @hanscharlz @storynzuri
.
Ilipoishia "Mama alipokuwa akiongea maneno yale alikuwa akitoa machozi nami ndipo nilipo msogerea karibu na kumbembeleza"
.
Mda ulipita na mama alisitisha kulia basi nilichukua jukumu la kuingia ndani ili niandae chakula cha pamoja kwani mama hakupenda mgeni aondoke bila hata ya kuweka kitu chochote mdomoni kwani ilikuwa Mira yetu mgeni akifika ni lazima aweke Baraka zake kwetu. Niliivisha chakula kwa mda mfupi tu kwani nilihitaji mgeni japo ale chakula nilicho kiandaa Mimi nilitaalisha meza na kutenga chakula ndipo nilipo chukua jukumu LA kuwakaribisha mama pamoja na mgeni (Yolanda).
Wote walifika mezani na wote kwa pamoja tulianza kula chakula nilicho kuwa nimewaandalia Mama pamoja na mgeni (Yolanda) waliendelea kupiga stori na stori walizokuwa wakipiga nje na waki simuliana zote zilikuwa pindi walipopotezana kipindi cha nyuma katikati ya stori hizo mgeni (Yolanda) alimwambia mama
Yolanda "kwanini nisimchukue binti yako nikaishi nae nyumbani kwangu kwani nilipojenga sasa Niko mwenyewe nyumba nzima na inabidi nikusaidie kwa kumsomesha Isabela mpaka atakapo fika elimu ya juu."
Mama "Nitashukuru sana rafiki yangu kwani Mimi hapa nime fanya kila njia ya kumtafutia mwanangu Ada ya kujiunga na shule kiukweli sikufanikiwa mpaka mda huu nilikuwa nimetokea kwenye miangaiko hiyo ya kutafuta pesa ya Ada. Nitashukuru tena sana kama utachukua jukumu LA kumtunza na kumsomesha mwanangu nani sina uwezo Wa kukulipa japo mungu yupo atakulipa yote na ndiye pekee awezaye."
Mgeni (Yolanda) usijali rafiki yangu tumetoka mbali sana kwani nilipo pata shida ulitia juhudi kunisaidia kipindi cha nyuma nami sita sita kwenye hili swala zito lililo kukumba rafiki yangu."
Nilifurahi sana kusikia mgeni (Yolanda) akinitaka Mimi ili akani someshe kiukweli sikutaka kuonesha Furaha yangu mbele zao kwani nilitaka hata akitaka kuondoka mda huo tuongozane nae mpaka anapo ishi ili tu nami nianze masomo mapema kwani wenzangu walikuwa wame fika mbali mno. Tulimaliza kula chakula ndipo mama aliniomba nijiandae ili tu mgeni akitaka kuondoka niongozane nae basi nilifanya hivyo hivyo kama mama alivyo sema kwani nilifanya upesi na nikawa tayari kwa safari.
About storynzuri
0 comments:
Post a Comment