Sehemu ya kwanza Mtunzi@hanscharlz @storynzuri
Nistori inayo muhusu binti Isabela .
Naitwa Isabela ni mzaliwa katika wilaya ya kwimba mkoani Mwanza nilizaliwa mwaka 1987 katika hospitali ya rufahaa bugando. Katika Familia yangu tumezaliwa watoto Wa wili Mimi pamoja na kaka yangu Gabriel na pia wazazi wetu walitulea kwa misingi ya dini na pia wazazi wangu na sisi kwa ujumla tuliishi kwa kutegemea kilimo. Hatukufanikiwa kuishi na wazazi wote kwani mzazi mmoja akitanguria mbele za haki R I P (BABA) mwaka 1999 kipindi hicho sito kisahau kwani baba alitutoka kwenye mazingira ya kututatanisha siku hiyo ilikuwa jumapili asubuhi na mapema baba aliamka na kwenda shambani basi Mimi pamoja na mama na kaka yangu Gabriel tulichelewa kwenda shambani kutokana na shuguri za asubuhi na tulipo maliza Kazi hizo tulielekea nasi tukaungane na baba yetu kwa siku hiyo. Tulifika shambani Mara moja hatukupoteza mda tulianza Kazi kwani tulikwisha muona baba yetu yuko ng'ambo ya pili akiendelea kulima. Masaa yalipita machache Mara gafra alipiga kelele na kunyamaza kimya wote tulishituka na hofu mwili mzima ilinitawala na ndipo tulielekea alipo baba yetu na tulipofika tulimkuta baba kalala chini na aongei tena yani alikuwa ameshatutoka. Tulikia sana kwani hatukujua nini kilimpata baba yetu na kupelekea mauti yake kwani alikuwa mtu mwenye afya nzuri siku hiyo. Basi tulifanya mipango ya mazishi ambayo haya kuchukua mda mwingi sana yalikamikika huku tukisaidiwa sana na wanakijiji na wana ndugu wachache walio fika kwenye msiba basi kila tulipo maliza mazishi kila mmoja alirudi na kuendelea na shuguri zake. Mama alikuwa mpweke sana kipindi hicho kwani ndiye aliyekuwa nguzo yetu na mboni yetu kwa kila kitu kwani ndiye aliyekuwa akitusomesha kwa bidii na kutusihi tusome tuutikomeze ujinga Mimi pamoja na kaka yangu Gabriel na alitutoka gafra sana kwani tulikuwa ndio tunaitimu masomo yetu darasa LA saba na ndicho kipindi tulikuwa tukisubili matokea ya kujiunga na sekondari. Matokeo yalikuja vizuri mimi pamoja na kaka yangu Gabriel tulichaguliwa kujiunga. Mama alipo pata taharifa ya kuwa sisi tumefanikiwa kujiunga na masomo ya sekondari mama..........?
About storynzuri
mmmmmmmmh
ReplyDelete